Pata taarifa kuu

Urusi: Watu kadhaa wakamatwa wakati wa maandamano dhidi ya agizo la rais Putin

Nchini Urusi, maandamano yamefanyika Jumatano hii, Septemba 21 kote nchini, baada ya Vladimir Putin kutangaza kuongeza askari wa akiba 300,000 kuunga mkono juhudi zake za vita nchini Ukraine.

Mwanamume mmoja akikamatwa wakati wa maandamano huko Moscow mnamo Septemba 21, 2022.
Mwanamume mmoja akikamatwa wakati wa maandamano huko Moscow mnamo Septemba 21, 2022. REUTERS - REUTERS PHOTOGRAPHER
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu walikamatwa katika angalau miji 20 tofauti, kulingana na kundi huru la waangalizi la OVD-Info. Walikuwa wakiandamana kufuatia tangazo, Jumatano asubuhi la Vladimir Putin, la kuongeza askari wa akiba 300,000 kwa ajili ya mashambulizi nchini Ukraine. 

Huko Moscow, watu kadhaa walikusanyika katikati mwa jiji, ambapo maafisa wa polisi walionekana kuwangojea. Vikosi vya usalama mara moja viliwakama watu kadaa, kulingana na waangalizi wa haki za binadamu, na barabara zilizingirwa haraka.

Wapinzani na wanaharakati wa kupinga vita wliitikia wito wa kuandamana kutoka kwa vuguvugu Vesna, lililotangazwa haraka baada ya rais wa Urusi kutangaza amri ya kuongeza idadi ya wanajeshi walio tayari kwa vita. Hii ni mara ya kwanza kwa Urusi kuajiri wanajeshi tangu Vita vya pili vya Dunia.

Katika siku zilizofuata uzinduzi wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, waandamanaji wasiopungua 16,000 walikamatwa wakati wa maandamano ya kupinga vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.