Pata taarifa kuu

Jamhuri za zamani za Soviet zatiwa wasiwasi baada ya Urusi kunyakua mikoa minne ya Ukraine

Baada ya Urusi kurasimisha majimbo manne ya Ukraine siku ya Ijumaa, Septemba 30, kufuatia kura za maoni zenye utata, wasiwasi bado unaongezeka katika jamhuri nyingi za zamani za Soviet. 

Nchi za zamani za Soviet wakati mwingine zimechukua misimamo dhidi ya Urusi juu ya suala la Ukraine, licha ya uwepo mkubwa wa jamii za Urusi. Hapa, watu wanaondoka katika jiji la Chmi nchini Urusi ili kuingia Georgia, Septemba 28, 2022.
Nchi za zamani za Soviet wakati mwingine zimechukua misimamo dhidi ya Urusi juu ya suala la Ukraine, licha ya uwepo mkubwa wa jamii za Urusi. Hapa, watu wanaondoka katika jiji la Chmi nchini Urusi ili kuingia Georgia, Septemba 28, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Ingawa nchi hizi zimeendelea kuwa washirika wa kimkakati wa Urusi, baadhi hazisiti kuikosoa Kremlin, hasa baada ya Kremlin kuhoji kuhusu kuanguka kwa USSR.

Miitikio kati ya jamhuri za zamani za Sovieti kwa kunyakuliwa kwa mikoa minne ya Ukraine bado haijawa mingi, kwani nyingi miongoni mwa jamhuri hizi bila shaka zeinajizuia kuonyesha misimamo yao. Hiyo ynaonekana, licha ya uvamizi wa Urusi, baadhi ya jamhuri hizi za zamani za Soviet zimefahamisha kwamba zinalaani unyakuzi huo wa Urusi ambao zimeutaja kuwa nikinyume cha sheria na usiokubalika.

Hiki ni kisa cha nchi ambayo kwa kawaida huwa makini zaidi kama Uzbekistan: taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Mambo ya Nje inakumbusha kuwa nchi hiyo inaheshimu mamlaka, uadilifu wa eneo na kanuni ya kutoingilia masuala ya ndani kutoka mataifa mengine.

nchi nyingne ambazo ni jamhuri za zamani za Soviet zinazounga mkono nchi za Magharibi, zimeonyesha upinzani wao. Moldova, kupitia sauti ya Rais Maia Sandu, imethibitisha kuwa Donetsk, Lugansk, Kherson, Zaporizhia na Crimea ni majimbo ya Ukraine. Georgia bado haijatoa msimamo wake, kwani mamlaka inazidi kuonyesha dalili za kuungana na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.