Pata taarifa kuu

Urusi kurasimisha unyakuzi wa maeneo ya Ukraine yaliyochukuliwa

Rais wa Urusi Vladimir Putin atarasimisha Ijumaa, Septemba 30 mjini Moscow unyakuzi wa Urusi wa maeneo ya Ukraine. Unyakuzi uliolaaniwa na jumuiya ya kimataifa, lakini ambao Moscow imetishia kuulinda hata kwa silaha za nyuklia. Hatua hiyo imetangazwa na Kremlin leo Alhamisi, kufuatia kura za maoni zilizopigwa katika maeneo yanayokaliwa na majeshi yanayoiunga mkono Urusi.

Wakazi wa Lugansk waweka bendera ya Urusi siku moja baada ya kumalizika kwa kura ya maoni kuhusu kunyakuliwa kwa eneo la Ukraine na Urusi, Septemba 28, 2022.
Wakazi wa Lugansk waweka bendera ya Urusi siku moja baada ya kumalizika kwa kura ya maoni kuhusu kunyakuliwa kwa eneo la Ukraine na Urusi, Septemba 28, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Kyiv, ikiungwa mkono na nchi za Magharibi na usambazaji wake wa silaha, imeapa kuendelea na mashambulizi yake na ambayo yamekuwa yakirudisha nyuma jeshi la Urusi kwa karibu mwezi mzima, na kumlazimu Vladimir Putin kuhamasisha mamia ya maelfu ya askari wa akiba.

Kremlin itaandaa sherehe siku ya Ijumaa ambapo unyakuzi wa mikoa ya Ukraine ya Donetsk na Lugansk (Mashariki), pamoja na Kherson na Zaporizhia (Kusini) utarasimishwa. "Sherehe ya kutia saini makubaliano ya kuingia kwa maeneo mapya katika Shirikisho la Urusi itafanyika kesho saa tisa saa za Urusi (sawa na saa sita saa za kimataifa) huko Kremlin," msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari. "Vladimir Putin atatoa hotuba kubwa katika hafla hii," ameongeza.

Mji mkuu wa Urusi ulikuwa ukijiandaa kwa sherehe za kuashiria kunyakuliwa kwa mikoa minne ya Ukraine, ambayo inakuja baada ya "kura za maoni" kulaaniwa na sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa.

Maafisa waliowekwa na Moscow katika mikoa ya Donetsk na Lugansk, Zaporizhia na Kherson, Kusini, tayari wako Moscow tangu Jumatano jioni, Septemba 28, kulingana na mashirika ya habari ya Kirusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.