Pata taarifa kuu

Unyakuzi wa Urusi nchini Ukraine: Volodymyr Zelensky afutilia mbali matakwa ya Moscow

Rais wa Urusi Vladimir Putin amerasimisha, Ijumaa hii, Septemba 30, unyakuzi wa Urusi wa majimbo manne yanayokaliwa na Urusi mashariki mwa Ukraine, na kutoa wito kwa Kyiv "kusimamisha uhasama mara moja" na kufanya mazungumzo. Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amemjibu rais wa Urusi kwamba matakwa yake hayakubaliki.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Septemba 29, 2022, wakati wa sherehe ya sherehe za ukumbusho nje kidogo ya mji wa Kyiv, ambapo wanajeshi wa Ujerumani wa Nazi waliwaua Wayahudi 30,000 mwaka wa 1941 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Septemba 29, 2022, wakati wa sherehe ya sherehe za ukumbusho nje kidogo ya mji wa Kyiv, ambapo wanajeshi wa Ujerumani wa Nazi waliwaua Wayahudi 30,000 mwaka wa 1941 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Kuchukuwa au la majimbo ya Ukraine, wakati Urusi sasa inamtaka aweke silaha chini, Bw. Zelensky amejibu akisema: hatajadiliana na Moscow hata kama Vladimir Putin bado atakaa madarakani kwa kipindi kirefu.

"Ukraine haitajadiliana na Urusi mradi tu Putin ni rais wa Shirikisho la Urusi. Tutajadiliana na rais mpya,” amesema kwenye video iliyowekwa mtandaoni na Kyiv.

Badala yake, rais Ukraine anatarajia kuongeza kasi. "Tunachukua hatua madhubuti kwa kutia saini matakwa ya Ukraine kuwa mwanachama wa NATO kuharakishwa," ameongeza.

Bw. Zelensky amependekeza kutekeleza mapendekezo ya dhamana ya usalama yaliyoandaliwa na Kyiv na washirika wake wa Magharibi. "Njia pekee ya kuleta amani katika eneo lote la nchi yetu ni kufukuzwa kwa wavamizi.

Ijumaa hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine pia alizungumza. Dmytro Kouleba amehakikishia kuwa nchi yake itaendelea kuongoza juhudi za vita ili kurudisha mali na maeneo yake yaliyochukuliwa na wavamizi.

"Hakuna mabadiliko kwa Ukraine: tunaendelea kukomboa maeneo yetu na watu wetu, kurejesha uadilifu wa eneo letu," amesema kwenye Twitter. Kulingana na waziri Dmytro Kouleba, Vladimir Putin "anajaribu kunyakua maeneo ambayo hayadhibiti kikamilifu". Na kwa kweli, hakuna jimbo lolote kati ya majimbo hayo manne yaliyonyakuliwa hivi karibuni na Moscow ambalo liko mikononi mwa vikosi vya Urusi.

Uamuzi wa kujiunga kwa Ukraine kwenye Muungano wa Atlantiki utahitaji umoja wa wanachama wa jumuiya hiyo ya kisiasa na kijeshi, amekumbusha, kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg.

Hata hivyo amesema NATO haitatambua maeneo haya kama sehemu ya Shirikisho la Urusi.

"Ukraine ina haki ya kurudisha maeneo haya ambayo sasa yamechukuliwa kwa nguvu na tutaiunga mkono ili iendelee kukomboa maeneo haya", ameongeza Bw. Stoltenberg, ambaye alizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.