Pata taarifa kuu

Ukraine: Putin atangaza uhuru wa majimbo ya Zaporizhia na Kherson

Rais wa Urusi ametangaza uhuru wa majimbo mawili ya Ukraine, Zaporizhia na Kherson wakati huu anapojiandaa kutangaza kuwa sasa ni maeneo ya Urusi, baada ya wakaazi ya majimbo hayo kushiriki kwenye kura ya maoni ambayo imelaaniwa na Ukraine na mataifa ya Magharibi. 

Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza wakati wa sherehe za kuadhimisha kujumuishwa kwa majimbo ya Ukraine kujiunga na Urusi, Red Square huko Moscow, Urusi, Ijumaa, Septemba 30, 2022. Kusainiwa kwa mikataba inayofanya mikoa minne kuwa sehemu ya Urusi kunafuatia kukamilika kwa "kura za maoni" zilizoratibiwa na Kremlin.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza wakati wa sherehe za kuadhimisha kujumuishwa kwa majimbo ya Ukraine kujiunga na Urusi, Red Square huko Moscow, Urusi, Ijumaa, Septemba 30, 2022. Kusainiwa kwa mikataba inayofanya mikoa minne kuwa sehemu ya Urusi kunafuatia kukamilika kwa "kura za maoni" zilizoratibiwa na Kremlin. AP - Gavriil Grigorov
Matangazo ya kibiashara

Majimbo mengine mawili ambayo Urusi sasa inadai ni sehemu ya ardhi yake ni Donetsk na Luhansk ambayo Putin anasema raia wake wameamua kuwa sehemu ya Urusi. 

Antonio Guteress ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anasema kitendo cha Urusi hakikukubaliki. 

Rais wa Marekani Joe Biden anaye amelaani hatua hiyo ya Urusi na kusema hawezi kutambua kwa vyovyote vile, majimbo hayo kuwa sehemu ya Moscow. 

Suala hili linatarajiwa kuchochea zaidi vita kati ya Ukraine na Urusi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.