Pata taarifa kuu

Marekani yatoa onyo la wazi dhidi ya Moscow

Marekani imelaani jaribio la ulaghai la Urusi kunyakua maeneo ya ardhi ya Ukraine, Joe Biden amesema katika taarifa yake, akilaani "ukiukaji wa sheria za kimataifa ambazo zinakanyaga Mkataba wa Umoja wa Mataifa".

Tổng thống Nga Vladimir Putin ngồi chờ thủ tướng Ấn Độ Narendra Modi trước cuộc hội đàm bên lề hội nghị Tổ chức Hợp tác Thượng Hải ở Samarcande, Uzbekistan ngày 16/09/2022, trong khi lâu nay ông Putin thường để cho các nhà lãnh đạo khác phải đợi mình.
Tổng thống Nga Vladimir Putin ngồi chờ thủ tướng Ấn Độ Narendra Modi trước cuộc hội đàm bên lề hội nghị Tổ chức Hợp tác Thượng Hải ở Samarcande, Uzbekistan ngày 16/09/2022, trong khi lâu nay ông Putin thường để cho các nhà lãnh đạo khác phải đợi mình. AP - Alexandr Demyanchuk
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani anaahidi kwamba Marekani "itaendelea kuunga mkono juhudi za Ukraine kurejesha udhibiti wa eneo lake".

Ikulu ya White House, Wizara ya Mambo ya Nje na ile ya  Fedha zimetangaza kupitishwa kwa vikwazo vipya Ijumaa hii, ambavyo vinalenga zaidi maafisa wa Urusi na tasnia ya ulinzi. Hii ni pamoja na wabunge kutoka Duma, Baraza la Bunge la Urusi, maafisa wa serikali na wauzaji wa vifaa kwa jeshi la Urusi.

Na mkuu wa diplomasia ya Marekani ametoa onyo jingine: kwa makubaliano na nchi za G7, Waziri wa Mambo ya Nje amehakikisha kwamba wale wote wanaotoa msaada wa kisiasa au kiuchumi kwa majaribio ya Urusi "kunyakua kinyume cha sheria sehemu za Ukraine watawekewa vikwazo vikali.

"Pia tunatoa onyo la wazi linaloungwa mkono na viongozi wa G7: tutawajibisha mtu yeyote, taasisi au nchi yoyote ambayo inatoa msaada wa kisiasa au kiuchumi kwa majaribio haramu ya Urusi ya kubadilisha hali ya maeneo nchini Ukraine," ameandika Antony Blinken katika taarifa.

G7 imetoa msimamo: wanachama wake "hawatatambua madai ya Urusi ya kunyakua" maeneo ya Ukraine, na kuahidi mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa saba yenye nguvu ya viwanda, pia katika taarifa kwa vyombo vya habari. "Tunalaani kwa kauli moja na vikali vita vya uchokozi vya Urusi dhidi ya Ukraine na kuendelea kwa Urusi kukiuka mamlaka ya kujitawala, uadilifu wa eneo na uhuru wa Ukraine. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.