Pata taarifa kuu

Ukraine: Kyiv na mikoa kadhaa yalengwa na mashambulizi ya angani ya Urusi

Jumatatu hii, Oktoba 17 asubuhi, mashambulizi kadhaa ya angani ya Urusi yamelenga miundombinu muhimu katika mikoa mitatu ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Kyiv.

Moja ya mitaa ya mjini Kyiv wakati wa shambulio la Oktoba 17, 2022.
Moja ya mitaa ya mjini Kyiv wakati wa shambulio la Oktoba 17, 2022. AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya yamesababisha "mamia ya maeneo" kutokuwa na umeme, Waziri Mkuu wa Ukraine, Denys Chmygal, ametangaza siku ya Jumatatu asubuhi. Takriban watu sita wameuawa katika mashambulizi mbalimbali katika miji ya Kyiv na Sumy. Nchi imetoa wito wa kutengwa kwa Urusi kutoka kwa kundi la nchi 20 zinazoongoza kiuchumi duniani G20.

Ni shambulio la ndege zisizo na rubani ambalo lilianza saa 12:23 asubuhi kwa saa za Ukraine (sawa na saa 9:23 usiku saa za kimataifa). Ndege kadhaa zisizo na rubani za Shahed-136 zilizotengenezwa na Iran zilionekana zikiruka juu ya mji mkuu Kyiv, anaripoti mwandishi wetu huko Kyiv, Stéphane Siohan. Na angalau nne kati ya ndege hizo zilianguka katikati ya mji wa Kyiv, katika wilaya ya Shevchenko, ambayo ni wilaya ya utawala, wilaya ya kati ya jiji. Inaonekana hasa kwamba pembezoni mwa kituo cha basi, na kituo cha kati mjini Kyiv vimelengwa na mashambulizi hayo.

Tuliona milipuko kadhaa ambayo ilitikisa katikati ya jiji, lakini pia maafisa wa polisi waliokuwepo hapo wakijaribu kufyatulia risasi kwa bunduki dhidi ya ndege zisizo na rubani. Wilaya hii ya kati ya Kyiv ilikuwa tayari ikilengwa wiki iliyopita wakati wa mfululizo wa mashambulizi mabaya ya Urusi kulipiza kisasi kwa mlipuko ambao uliharibu kwa kiasi kikubwa daraja la Crimea.

Angalau majengo manne, yakiwemo ya ghorofa, yaliharibiwa na milipuko hii ya ndege zisizo na rubani. Kulingana na meya wa mji wa Kyiv, shambulio la Urusi katika mji huo liligharimu maisha ya mtu mmoja na watatu kujeruhiwa. Mashambulizi ya Urusi "haitaweza kuwasambaratisha" Waukraine, amesema Rais Volodymyr Zelensky kwa upande wake baada ya mashambulizi haya kwenye mji mkuu.

"Usiwalengi raia na mali zao"

Volker Türk, ambaye alianza majukumu yake kama Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa mnamo Oktoba 17, amehimiza "kutolenga malengo ya kiraia". Wakati diplomasia ya Ukraine inataka vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran inayotuhumiwa kutoa ndege zisizo na rubani za vilipuzi kwa Urusi.

Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Chmygal pia amezungumzia "mashambulizi mengine ya makombora" kwenye mikoa ya Dnipropetrovsk (katikati-mashariki) na Sumy (kaskazini-mashariki). "Mamia ya maeneo hayana umeme," ameongeza. "Huduma zote kwa sasa zinafanya kazi [...] kurejesha umeme", amesema, akiwaomba wakazi wa mikoa hii mitatu "kubana matumizi ya umeme, hasa nyakati muhimu ".

Wazima moto baada ya mgomo wa ndege zisizo na rubani huko Kyiv, Oktoba 17, 2022.

Wazima moto baada ya mgomo wa ndege zisizo na rubani mjini kyiv, Oktoba 17, 2022. © Efrem Lukatsky / AP

Urais wa Ukraine ulithibitisha, kwa upande wake, kwamba "kuna waliokufa na waliojeruhiwa" kufuatia migomo ya Urusi katika eneo la Sumy. Katika mkoa wa Dnipropetrovsk, "askari wetu walirusha makombora matatu ya adui", aliongeza rais, lakini "roketi moja iligonga usanidi wa miundombinu ya nishati", alibainisha.

Saa chache kabla ya milipuko iliyoukumba mji wa Kyiv, ndege zisizo na rubani za zenyz vilipuzi ziliruka juu ya matangi yaliyojaa mafuta ya alizeti katika bandari ya kusini ya Mykolaiv.

Kwa upande wake, jeshi la Urusi linadai kuwa limefikia malengo yake yote nchini Ukraine. "Vikosi vya jeshi la Urusi vimeendelea kufanya mashambulizi ya masafa marefu ya anga na baharini kwa silaha zenye usahihi wa hali ya juu dhidi ya makao makuu na vifaa vya mfumo wa nishati nchini Ukraine. Vituo vyote vilivyokusudiwa vimelengwa na mashambulizi, "Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kwenye Telegraph.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.