Pata taarifa kuu

Wakuu wa Nchi 44 wakutana mjini Prague kwa uzinduzi wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya

Viongozi 44 wa Nchi na Serikali wanakutana kuanzia Alhamisi hii, Oktoba 6 katika Kasri la Prague, nchini Jamhuri ya Czech. Watashiriki katika uzinduzi wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya (EPC), muundo mpya ulioanzishwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika katika majira ya baridi 2022 na uliyokusudiwa kuleta pamoja nchi za bara hilo, kuhusiana na vita ambavyo Urusi inaendesha nchini Ukraine.

Wakuu wa Nchi 44 wanakutana katika Kasri la Prague siku ya Alhamisi tarehe 6 Oktoba kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya.
Wakuu wa Nchi 44 wanakutana katika Kasri la Prague siku ya Alhamisi tarehe 6 Oktoba kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya. © Getty Images - Fandrade
Matangazo ya kibiashara

Mpango huo ulianzishwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na mkutano huu wa kwanza wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya unafanyika Prague, kwa sababu Jamhuri ya Czech kwa sasa inashikilia uenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya, ameripoti mwandishi wetu huko Prague, Alexis Rosenzweig.

Lengo lake ni kufanya kazi ili kuimarisha usalama na utulivu kwani vita vya Ukraine vimeingia mwezi wa nane sasa. Mada mbili zitakuwa kwenye mpango wa meza za pande zote kwa washiriki arobaini na wanne: nishati na Tabia nchi, amani na usalama, anaelezea mwandishi wetu Anastasia Becchio. Ni msaada gani wa ziada utakaopewa Ukraine? Jinsi ya kulinda miundombinu muhimu? Swali la papo hapo, baada ya milipuko kwenye mabomba ya gesi ya Nord Stream katika Bahari ya Baltic. Wasiwasi huu pia utakuwa kwenye ajenda ya mkutano usio rasmi wa kilele wa EU siku ya Ijumaa.

Mbali na nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU), mataifa mengine kumi na saba yamealikwa kwenye uzinduzi wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya. Miongoni mwa wageni wanaotarajiwa: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ambaye atazungumza kwa njia ya video, Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss, na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye uwepo wake unazua mjadala.

Ushiriki wa Uturuki wazua mjadala

Emmanuel Macron hakuficha ukweli kwamba mwaliko wa Uturuki - ambayo hata hivyo ni nchi kongwe zaidi ya mgombea wa uanachama wa Umoja wa Ulaya - ilibidi kujadiliwa kati ya Nchi Wanachama kabla ya kukubaliwa kushiriki mkutano huo, anaripoti mwandishi wetu huko Istanbul. , Anne Andlauer. Recep Tayyip Erdogan hajaonyesha shauku yoyote kwa muundo huu mpya, akithibitisha kuwasili kwake siku tano kabla ya mkutano huo.

Kusita huku kunatokana hasa na kutokuwa na uhakika unaozingira mradi wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya na maslahi yake kwa Uturuki. Ingawa EU imekanusha, Ankara inahofia chochote ambacho kinaweza kutumika kama mbadala wa uanachama. Sio kwamba hii iko kwenye ajenda: imezuiwa kwa zaidi ya miaka kumi.

Kutokuwa na imani kwa nchi kadhaa

Ingawa Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, amethibitisha kwamba lengo lake lilikuwa "kuimarisha usalama, utulivu na ustawi wa Ulaya kwa ujumla", miji mikuu kadhaa haikuficha mashaka yao, hata kutoamini kwao mradi huu mpya, anaripoti mwandishi wetu huko Prague, Alexis Rosenzweig. Baadhi ya nchi, ikiwa ni pamoja na Uturuki, yananusa mkakati unaolenga kupunguza kasi ya mchakato wa upanuzi wa EU, nchi zingine hazitaki kushitrkiana na majirani ambao wana mgogoro nao - wa siri au wa wazi.

Rais wa Uturuki pia anaonekana kusitasita kuhusu kujiunga na "kambi dhidi ya Putin", kama wengine wanavyoona au wangependa kuona. Bwana Erdogan anapenda sana uhusiano wake na kiongozi wa Urusi, ambaye anajivunia kuwa mpatanishi mkuu tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine. Alitoa maoni machache sana kuhusu ushiriki wake katika mkutano huu, isipokuwa kueleza nia yake ya kukutana na Waziri Mkuu wa Armenia, Nikol Pashinian.

Jumuiya hii ya Kisiasa ya Ulaya inakumbusha mradi ulioghairiwa wa Shirikisho la Ulaya uliozinduliwa mnamo 1991 na François Mitterrand na Vaclav Havel, Rais wa Jamhuri ya Czech ambaye aliacha alama yake kwenye Jumba la Prague ambapo mkutano huu wa kwanza unafanyika, na kufuatiwa Ijumaa na mkutano wa kilele wa nchi 27, wanachama wa EU.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.