Pata taarifa kuu

G7 inatoa wito kwa IMF kutoa msaada kwa Ukraine kabla ya mwisho wa mwezi Machi

Mawaziri wa fedha wa kundi la nchi zilizotawi kiuchumi, G7, wamelitaka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kutoa kifurushi kipya cha msaada kwa Ukraine kufikia mwisho wa mwezi Machi, kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa Alhamisi baada ya mkutano huko Bangalore, India.

G7 inatoa imeiomba IMF kutoa msaada kwa Ukraine kabla ya mwisho wa mwezi Machi ili kukabiliana na matatizo yanayoikabili.
G7 inatoa imeiomba IMF kutoa msaada kwa Ukraine kabla ya mwisho wa mwezi Machi ili kukabiliana na matatizo yanayoikabili. © Aleph news
Matangazo ya kibiashara

"Tunazihimiza IMF na Ukraine kuweka mpango kabambe, wenye kuaminika, utakaofadhiliwa kikamilifu na masharti yanayofaa kufikia mwisho wa Machi 2023," waraka huo unasema.

Wakati huo huo Ujerumani imeandaa msururu wa hatua zinazolenga kuziba mianya ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Moscow, hususan kuzuia bidhaa zilizowekewa vikwazo kuendelea kuingia Urusi kupitia ya nchi tatu.

Berlin itashinikiza hatua hizo ziwe sehemu muhimu ya duru ya 11 ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Moscow, wizara ya uchumi imesema leo Alhamisi. Kifurushi cha 10 cha vikwazo vya Umoja wa Ulaya kitatangazwa siku ya Ijumaa, siku ya kumbukumbu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.