Pata taarifa kuu

Uingereza: Liz Truss achukuwa mikoba ya Boris Johnson

Liz Truss amechaguliwa Jumatatu, Septemba 5, kuchukuwa nafasi ya kiongozi wa Chama cha Conservative, mbele ya mpinzani wake Rishi Sunak, kuchukua nafasi ya Boris Johnson kama kiongozi wa Tories na serikali ya Uingereza. Ataende kesho Jumanne hadi Scotland kukutana na Malkia Elizabeth, ambaye atamtaka aunde serikali.

Liz Truss, ambaye ni kiongozi mpya wa Chama cha Conservative, anajiandaa kutoa hotuba yake. Septemba 5, 2022.
Liz Truss, ambaye ni kiongozi mpya wa Chama cha Conservative, anajiandaa kutoa hotuba yake. Septemba 5, 2022. REUTERS - HANNAH MCKAY
Matangazo ya kibiashara

Liz Truss amechaguliwa na wanachama wa Chama cha Conservative nchini Uingereza kuwa Waziri Mkuu na kumrithi Boris Johnson, chama cha walio wengi nchini Uingereza kimetangaza Jumatatu. Haishangazi, Waziri wa Mambo ya Nje mwenye umri wa miaka 47 ameshinda kwa tofauti kubwa (57%) dhidi ya mwenzake wa zamani wa fedha, Rishi Sunak (43%), kulingana na matokeo yaliyotangazwa na Graham Brady, aliyehusika na kuandaa uchaguzi wa ndani uliotokana na kujiuzulu kwa Boris Johnson mapema mwezi wa Julai.

Waziri Mkuu mpya ameahidi, katika taarifa zake za kwanza, "mpango wa ujasiri" wa kupunguza kodi na kuongeza ukuaji, katikati ya gharama ya shida ya maisha. "Nitatekeleza mpango bora wa kupunguza kodi zetu na kuongeza ukuaji wa uchumi wetu," amesema baada ya ushindi wake kutangazwa, pia akiapa kukabiliana na mlipuko wa bei ya nishati kwa kaya na matatizo ya "muda mrefu" yanayohusu vifaa vya nishati.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema anatazamia kufanya kazi "katika nyakati hizi ngumu" na Liz Truss. "Uingereza na Ujerumani zitaendelea kufanya kazi kwa karibu, kama washirika na kama marafiki," Kansela ameongeza kwenye ukurasa wake wa twitter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.