Pata taarifa kuu
Uingereza - Siasa

Uingereza : Waziri mkuu Boris Johnson asisistiza hatajiuzulu

Nchini Uingereza, Waziri Mkuu Boris Johnson ameendelea kusisitiza kuwa hatojiuzulu licha ya kuendelea kupaya shinikizo za kumtaka afanye hivyo kufuata kashfa mbalimbali zinazoiandama serikali, na kusababisha kujiuzulu kwa baadhi ya  Mawaziri wake, na maafisa wengine wa serikali.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson AP - Hollie Adams
Matangazo ya kibiashara

Johnson amewambia, wabunge kwamba ataendelea kutekeleza majukumu yake, licha ya shinikizo za kumtaka ajiuzulu, kufutia kuongezeka kwa idadi ya mawaziri wanaojiuzulu na maafisa wengine wa serikali wanaomtuhumu Johnson kwa kukosa kuwachukulia hatua maafisa wa serikali yake wanaotuhumiwa kuhusika katika unyanyasaji wa kingono.

Aidha mawazi kadhaa wakiwemo wandani wake Johnson, kama vile  waziri wa uchukuzi  Grant Shapps,   wanatarajiwa kuandaa kikao naye kumshawishi ajiuzulu.

katika hatua nyingine Johnson amemfuta kazi mmoja wa mawaziri wake Michael Gove, huku chama chake cha Conservative kikitarajiwa kukutana wiki ijayo kuangalia upya kanuni za chama ili kuitisha kura ya kukosa imani naye, wakati ou huo waziri mweingine Simon Hart, pia amejiuzulu.

 

 

 

 

 

 

 

.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.