Pata taarifa kuu
Uingereza - Siasa

Uingereza : Boris Johnson ajiuzulu wadhifa wa kiongozi wa chama cha Conservative

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amejiuzulu kama kiongozi wa chama tawala cha Conservative, hatua yake ikitoa nafasi ya chaguliwa kwa waziri mkuu mpya, baada ya mawaziri kadhaa wa serikali yake kujiuzulu.

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson
Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson AP - Hollie Adams
Matangazo ya kibiashara

Johnson mwenye miaka 58, ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu hadi pale waziri mkuu mpya atapoteuliwa.

Muda wa kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya kutatangazwa juma lijalo.

Johnsona  baada ya kkuhudumu kwa miaka mitatu ambayo imekubwa na masaibu mengi ikiwemo kujiondoa kwa Uingereza kwa umoja wa Ulaya na janga la Uviko 19, hatimaye amekubali kuondoka afisini licha ya wali kusisitiza hangejiuzulu.

Uteuzi wa kiongozi mpya wa chama cha Conservative, utafanyika kufikia mwishoni wa mwezi Agosti, waziri mkuu mpya akitarajiwa kutangazwa mwezi Oktoba.

Johnson amesema  anasikitika kuiacha kazi nzuri zaidi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.