Pata taarifa kuu
Uingereza - Siasa

Uingereza : Boris Johnson kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative

Waziri mkuu Boris Johnson anarajiwa kujiuzulu kama kiongozi wa chama tawala cha Conservative baadaye leo, lakini atandelea kuhudumu kama waziri  hadi baadaye mwaka huu.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson REUTERS - HENRY NICHOLLS
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi mpya wa chama cha Conservative anatarajiwa kuchaguliwa na kuanza kuhudumu kama waziri mkuu kufikia mwisho wa mwezi Oktoba.

Hatua hii inajiri siku moja tu baada ya waziri mkuu Johnson kusisitiza kuwa hatajiuzulu kutokana na tuhuma ambazo zimekuwa zikimuandama.

Johnson alikuwa amewambia wabunge kwamba ataendelea kutekeleza majukumu yake, licha ya shinikizo za kumtaka ajiuzulu, kufutia kuongezeka kwa idadi ya mawaziri wanaojiuzulu na maafisa wengine wa serikali wanaomtuhumu Johnson kwa kukosa kuwachukulia hatua maafisa wa serikali yake wanaotuhumiwa kuhusika katika unyanyasaji wa kingono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.