Pata taarifa kuu

Gazprom yasitisha utoaji wa gesi kwa Poland na Bulgaria

Kampuni ya nishati ya Urusi, Gazprom, imetangaza Jumatano kwamba imesitisha utoaji wa gesi kwa Bulgaria na Poland, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ambazo hazijafanya malipo kwa fedha za Urusi.

Ofisi za kampuni kubwa ya gesi ya Gazprom huko Moscow, Septemba 2021.
Ofisi za kampuni kubwa ya gesi ya Gazprom huko Moscow, Septemba 2021. © AFP - ALEXANDER NEMENOV
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, Gazprom imesema imeijulisha kampuni ya Bulgaria ya Bulgargaz na kampuni ya Poland ya PGNiG kuhusu "kusitishwa kwa utoaji wa gesi kuanzia Aprili 27 hadi malipo yamefanywa" kwa fedha za Urusi. Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema mwezi uliopita kwamba Urusi itakubali tu malipo ya usafirishaji wa gesi kwa sarafu yake ya kitaifa.

Ukraine yatangaza kudhibitiwa kwa maeneo kadhaa na vikosi vya Urusi Mashariki

Jeshi la Ukraine limetambua kusonga mbele kwa vikosi vya Urusi mashariki mwa nchi, kwa kudhibiti miji midogo kadhaa katika mkoa wa Kharkiv na Donbass.

Vikosi vya Urusi vinasonga mbele kutoka Izium, ambayo tayari iko chini ya udhibiti wao, kuelekea Lyman na karibu na Severodonetsk, moja ya miji mikubwa katika eneo hilo, Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema katika ripoti yake ya asubuhi.

Mapema Jumatano asubuhi, vikosi vya Ukraine viliripoti shambulio la makombora la Urusi likilenga vijiji vidogo vilivyo mstari wa mbele katika vita katika mkoa wa Donbass. Ukraine inadai kuwa maeneo ya kiraia yanalengwa kiholela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.