Pata taarifa kuu

Washington na washirika wake wakutana Ramstein kuimarisha uwezo wa kijeshi wa Kyiv

Marekani imeandaa mkutano na washirika 40 katika kambi ya ya jeshi la Marekani huko Ramstein nchini Ujerumani ili kuratibu juhudi zao za kuunga mkono zana za kijeshi za Ukraine na kuwezesha Kyiv kukabiliana dhidi ya uvamizi wa Urusi. Tangazo thabiti zaidi lilihusu hatua ya Ujerumani kukubali kutoa vifaru , haya ni "maendeleo makubwa" amesema Waziri wa Ulinzi wa Marekani.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akionyesha ishara anapohutubia mkutano wa wanahabari baada ya mkutano na wanachama wa Kundi la Ushauri wa Usalama la Ukraine katika Kambi ya jeshi la Wanahewa la Marekani ya Ramstein magharibi mwa Ujerumani, Aprili 26, 2022.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akionyesha ishara anapohutubia mkutano wa wanahabari baada ya mkutano na wanachama wa Kundi la Ushauri wa Usalama la Ukraine katika Kambi ya jeshi la Wanahewa la Marekani ya Ramstein magharibi mwa Ujerumani, Aprili 26, 2022. AFP - ANDRE PAIN
Matangazo ya kibiashara

"Matokeo ya mzozo huu yanategemea watu waliokusanyika katika ukumlbi huu leo." Mkuu wa jeshi la Marekani Mark Milley amebaini kwa maneno machache wakati wa mkutano wa Ramstein umuhimu wa mkutano huo. Marekani na washirika wake - nchi arobaini zimewakilishwa leo katika kambi ya kijeshi ya Ramstein nchini Ujerumani - wanataka kuunda kundi la mawasiliano litakalokutana kila mwezi. Lengo: kuimarisha uwezo wa kijeshi wa Ukraine.

Pamoja na nchi za Ulaya, wanachama wa NATO nchi ambazo si wanachama, mataifa kama vile Australia, Israel na Qatar yameshiriki leo mkutano huo. Wiki chache zijazo itakuwa muhimu kwa Ukraine na kwa hivyo kuna dharura.

Siku ya Jumatatu Marekani ilitangaza kutoapesa zingine karibu dola milioni 700 kama msaada wa kijeshi kwa Kyiv. Berlin, ambayo imeshutumiwa sana hadi sasa kwa kuzuia uwasilishaji wa silaha nzito, imetangaza kuwa karibu vifaru hamsini vya Cheetah vilivyotengenezwa kwa ulinzi wa anga vitakabidhiwa Kyiv. Misheni za mafunzo kwa vikosi vya Ukraine zitapangwa nchini Ujerumani.

Rheinmetall pia imeomba serikali ruhusa ya kuuza nje takriban mizinga 200 na magari ya kivita. Berlin inataka kujibu ombi hili haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.