Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Urusi yalaani shambulio jipya kwenye ardhi yake

Jeshi la Ukraine limetambua kusonga mbele kwa vikosi vya Urusi mashariki mwa nchi, kwa kudhibiti miji midogo kadhaa katika mkoa wa Kharkiv na Donbass.

Mapema mwezi huu, Urusi iliishutumu Ukraine kwa kuhusika na shambulio la ghala la mafuta katika Jimbo la Belgorod.
Mapema mwezi huu, Urusi iliishutumu Ukraine kwa kuhusika na shambulio la ghala la mafuta katika Jimbo la Belgorod. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka iliyojitenga ya Moldova huko Transnistria imeshutumu "shambulio la kigaidi" dhidi ya kitengo cha kijeshi Jumanne asubuhi, pamoja na milipuko kwenye mitambo miwili ya redio na Wizara ya Usalama wa Umma Jumatatu jioni. Matukio hayo yanazidisha hofu ya kusambaa kwa mzozo nchini Moldova, ambayo imeamua kuitisha kwa dharura baraza lake la usalama la taifa. Ukraine inaishutumu Urusi kwa kutaka "kuyumbisha" usalama wa Moldova. Mamlaka ya Moldova inatoa wito kwa utulivu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov siku ya Jumanne, kisha Rais Vladimir Putin mjini Moscow. Alisema anatafuta njia za kupata "suluhisho la amani" haraka iwezekanavyo. Kulingana na Umoja wa Mataifa, Vladimir Putin anakubali msaada kutoka kwa Umoja wa Mataifa kwa kuwahamisha raia kutoka kiwanda cha Azovstal huko Mariupol.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeionya Uingereza dhidi ya "jibu sawia" mara moja ikiwa serikali ya Uingereza itaendelea "chokocho zake za moja kwa moja" kutoka Ukraine kwa kufanya mùashambulizi nchini Urusi.

Wakati huo huo Kampuni ya Urusi ya Gazprom imesitisha utoaji wa gesi kwa Bulgaria na Poland "kuanzia Aprili 27 na hadi malipo yamefanywa" kwa fedha za Urusi. Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema mwezi uliopita kwamba Urusi itakubali tu malipo ya usafirishaji wa gesi kwa sarafu yake ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.