Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Ufaransa kumchagua rais wake mpya katika duru ya pili

Mamilioni ya wapiga kura nchini Ufaransa, wanapiga kura Jumapili hii Aprili 24, kumchagua rais katika duru ya pili ya uchaguzi, unaowakutanisha rais Emmanuel Macron na mwanasiasa wa siasa za mrengo wa kulia, Marine Le Pen, baada ya kushindwa kupatikana mshindi katika duru ya kwanza, wiki mbili zilizopita.

Wafaransa wanapiga kura kumchagua rais wao.
Wafaransa wanapiga kura kumchagua rais wao. AFP - LOIC VENANCE
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu wa marudio unafanyika kwa sababu katika duru ya kwanza wiki mbili zilizopita, hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Rais Macron kutafuta muhula wa pili, anapewa nafasi kubwa ya anayeibuka mshindi, baada ya wadadisi wa siasa kusema vema kwenye mjadalo wa Televisheni wiki hii dhidi ya Le Pen.

Hata hivyo, uchaguzi huu pia unaelezwa kuwa na ushindani mkali kinyume na ilivyokuwa mwaka 2017, huku Marine Le Pen akisema ana imani ya kuibuka mshindi licha ya sera zake, ambazo zinaonekana kuwa rafiki hasa barani Ulaya.

Vituo vya kupigia kura, vitafunguliwa kuanzia mbili asubuhi saa za Paris na kufungwa baada ya saa 12 na matokeo yatafamika baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.