Pata taarifa kuu

Kenya: Joto la kisiasa laendelea kutokota kuelekea uchaguzi

Nchini Kenya, naibu rais William Ruto anayeongoza muungano wa Kenya Kwanza, amesaini mkataba wa ushirikiano kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti. 

William Ruto, Makamu wa rais wa Kenya Jumanne Mei 14 mwaka 2013.
William Ruto, Makamu wa rais wa Kenya Jumanne Mei 14 mwaka 2013. REUTERS/Lex van Lieshout/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ruto atakayewania urais kupitia muungano huo unaoundwa na zaidi ya vyama 10, amesema muungano huo utaleta mabadiliko nchini Kenya ukiingia madarakani. 

Katika hatua nyingine, muungano wa Azimio One Kenya, ambao mgombea wake ni kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga, umekanusha madai kuwa kuna mpasuko kati ya vyama mbalimbali. 

Kazi kubwa iko mbele ya miungano hiyo miwili ni kumtafuta wagombe wenza kuelekea kuanza kwa kampeni rasmi mwezi ujao. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.