Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Kenya: Wagombea katika uchaguzi wa urais waanza kuwatafuta wagombea wenza

Wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais nchini Kenya, Raila Odinga na William Ruto, bado hawajawateua wagombea wenzao, kuelekea makataa ya uteuzi huo, mwisho wa mwezi huu

Katika moja ya mitaa ya Nairobi, Kenya, Mei 3, 2021.
Katika moja ya mitaa ya Nairobi, Kenya, Mei 3, 2021. SOPA Images/LightRocket via Gett - SOPA Images
Matangazo ya kibiashara

Wachambuzi wa siasa wanaona uteuzi huu unachukua muda kwa sababu, wagombea ni sharti wawe makini kumpata mgombea mwenza ambaye atawavutia wapiga kura. 

Katika muungano wa Odinga na Azimio One Kenya, vuguvugu la wanawake katika muungano huo sasa linataka Martha Karua kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Kenya inajitayarisha kwa uchaguzi wake mkuu wa Agosi tarehe 9 mwaka huu na jambo moja kubwa ambalo limejitokeza wazi na ambalo linazidi kuzungumziwa ni kujipata kwa familia tatu kubwa za kisiasa katika mrengo mmoja kwenye uchaguzi huo.Familia hizo zimekuwa nyuso zinazotambulika katika siasa za Kenya tangu ijinyakulie uhuru na yamkini vizazi vya wanasiasa hao watangulizi bado vipo kati kati ya uchaguzi wa mwaka huu.

Siasa za Kenya kwa miaka mingi tangu nchi hiyo ipate uhuru wake mwaka wa 1963 zimeegemea familia za Mzee Jomo Kenyatta na Jaramogi Oginga Odinga, mashujaa wawili wa vita vya ukombozi, ambao miaka miwili baada ya uhuru walitofautiana na kuwa mahasimu wakuu wa kisiasa.

Ijapokuwa Daniel arap Moi, alikuwa rais wa pili wa Kenya aliyekaa mamlakani kwa muda mrefu zaidi - miaka 24, na rais wa tatu, Mwai Kibaki ambaye alikuwa madarakani kati ya 2002-2013, unapofuatilia hisia na siasa za Kenya, taswira inayotawala ni kati ya familia mbili- ya Kenyatta na ile ya Odinga.Maajuzi mtoto wa rais wa pili Daniel Moi ,Gideon Moi naye amejipata katika muungano wa Azimio la Umoja ambao unamuunga mkono Raila Odinga kumrithi rais Uhuru Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.