Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Kenya: Matukio kadhaa yazua hofu ya ghasia wakati wa kipindi cha uchaguzi

Usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano mjini Mombasa, magari mawili yalimfyatulia risasi 22 Ali Mwatsau, mgombea ubunge katika chama cha William Ruto, na kujeruhiwa vibaya. Tukio hilo linajiri huku kukiwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa ghasia katika kipindi cha uchaguzi, ambapo siku chache tu zilizopita mgombea urais Raila Odinga alilengwa na shambulizi.

Ijumaa iliyopita, shambulizi lilimlenga Raila Odinga anayewania kiti cha urais.
Ijumaa iliyopita, shambulizi lilimlenga Raila Odinga anayewania kiti cha urais. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Katika ukurasa wake wa Twitter, William Ruto Jumatano alikashifu "jaribio la mauaji" dhidi ya mgombea wake Ali Mwatsau. Sbabu za shambulio hilo hazijajulikani. Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya alitoa wito wa kuachana na uvumi na kuzingiziana kwa hiki ama kile, huku akiwataka raia kusubiri hitimisho la uchunguzi.

Ijumaa ya wiki iliyopita, helikopta ya Raila Odinga ilishambuliwa kwa mawe na wafuasi wa kambi nyingine, wakati mwanasiasa huyo alipokuwa akiondoka kwenye mazishi. Kufuatia hali hiyo, viongozi kadhaa wa kisiasa walilaani tukio hilo akiwemo William Ruto na Uhuru Kenyatta. Rais wa Kenya alitoa wito kwa viongozi wa kisiasa kufanya kampeni kwa amani.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Fred Matiang'i alithibitisha Jumanne kwamba shambulio hilo lilipangwa kimakusudi, akibainisha kuwa washukiwa walikamatwa wakiwa na pesa mikononi. Mbele ya Bunge, alikemea baadhi ya vitendo vya kampeni ambavyo alisema vinazidisha mivutano, kama vile ununuzi wa kura au usafiri wa vijana wanaolipwa kuhudhuria mikutano ya kisiasa. Alitaja mikutano mitatu ya awali ambapo William Ruto alikabiliwa na vitendo vya unyanyasaji.

Hata hivyo, alithibitisha kuwa nchi iko tayari kuhakikisha usalama wa uchaguzi huo. Ikiwa hali inatia wasiwasi, ni kwa sababu ghasia za baada ya uchaguzi zinatokea mara kwa mara nchini Kenya. Raia nchini Kenya wanakumbuka hasa machafuko yaliyofuatia uchaguzi wa mwaka 2007, ambapo zaidi ya watu 1,000 waliuawa na laki kadhaa kuyatoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.