Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais Ufaransa: 26.41% ya wapiga kura waliojitokeza mchana

Wapiga kura waliojitokeza katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa hadi saa 12 mchana wamefikia kwa 26.41%, karibu chini ya pointi mbili mwaka wa 2017 (28.23%) wakati Emmanuel Macron akichukuana na Marine Le Pen.

Wapiga kura wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais mwaka 2022 huko Paris, Aprili 24, 2022.
Wapiga kura wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais mwaka 2022 huko Paris, Aprili 24, 2022. © PIROSCHKA VAN DE WOUW/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu wa marudio unafanyika kwa sababu katika duru ya kwanza wiki mbili zilizopita, hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Rais Macron kutafuta muhula wa pili, anapewa nafasi kubwa ya anayeibuka mshindi, baada ya wadadisi wa siasa kusema vema kwenye mjadalo wa Televisheni wiki hii dhidi ya Le Pen.

Hata hivyo, uchaguzi huu pia unaelezwa kuwa na ushindani mkali kinyume na ilivyokuwa mwaka 2017, huku Marine Le Pen akisema ana imani ya kuibuka mshindi licha ya sera zake, ambazo zinaonekana kuwa rafiki hasa barani Ulaya.

Vituo vya kupigia kura, vitafunguliwa kuanzia mbili asubuhi saa za Paris na kufungwa baada ya saa 12 na matokeo yatafamika baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.