Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Emmanuel Macron na Marine Le Pen kupambana kwenye mdahalo a televisheni

Nchini Ufaransa, wagombea wawili wa urais siku ya Jumapili rais Emmanuel Macron na Marine Le Pen leo wanashiriki kwenye mdahalo wa Televisheni, unaosubiriwa na mamilioni ya wapiga kura nchini humo.

Marine Le Pen mgombea urais kupitia chama cha Rassemblement national na Emmanuel Macron, watamenyana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, Aprili 24, 2022.
Marine Le Pen mgombea urais kupitia chama cha Rassemblement national na Emmanuel Macron, watamenyana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, Aprili 24, 2022. © REUTERS/Sarah Meyssonnier/Benoît Tessier/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Macron na Le Pen wanatarajiwa kupambana vikali, huku wakitazmwa na mamilioni ya Wafaransa na watu wengine duniani, huku kila mmoja akipata nafasi ya kueleza sera zake. 

Mdahalo huu unafanyika wakati huu kura za maoni zikionesha kuwa, kutakuwa na ushindani mkali siku ya Jumapili, na wapiga kura ambao hawajaamua watampigia nani kura, wana nafasi ya kipekee kufanya uamuzi wao. 

Aidha, pande zote za rais Macron na Le Pen, zimeshtumiwa kwa kumkataa mtangazaji  maarufu wa kituo cha France 2, Anne-Sophie Lapix, kuongoza mdahalo huo, kutokana na uwezo wake wa kuwauliza wanasiasa maswali magumu. 

Kura ya maoni kutoka Shirika la Ipsos inaonesha kuwa, Macron ana nafasi ya kushinda katika mzunguko wa pili kwa asimilia 56.5 dhidi ya mpinzani wake Le Pen anayepewa asilimia kati ya 44 na 47. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.