Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Ufaransa : Kampeni za uchaguzi zaendelea kuelekea duru ya pili ya uchaguzi wa urais

Nchini Ufaransa, wagombea wawili kwenye kiti cha urais, rais anayemaliza muda wake Emmanuel Macron na Marine Le Pen wameingia katika wiki ya mwisho ya kampeni kuelekea duru ya pili ya uchaguzi siku ya Jumapili.

Emmanuel Macron na Marine Le Pen watamenyana Jumapili Aprili 24, 2022 katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Ufaransa.
Emmanuel Macron na Marine Le Pen watamenyana Jumapili Aprili 24, 2022 katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Ufaransa. © Montage RFI - Reuters/AP
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wanarejelea tena kampeni hivi leo, baada ya mapumziko ya sikukuu ya Pasaka mwishoni mwa wiki iliyopita, kuomba kupigiwa kura. Le Pen atakuwa Normandy Kaskazini mwa Ufaransa huku Macron akitarajiwa kuhojiwa na vyombo mbalimbali ya habari hivi leo.

Mbali na kampeni za leo na kesho siku ya Jumatano, Macron na Le Pen watapambana katika mdahalo utakaopeperushwa mubashara na vyombo vingi vya habari nchini humo. 

Uchaguzi wa Jumapili, unaleta kumbukumbu ya mwaka 2017 wakati wawili hawa walimenyena tena katika mzungulo wa pili, na Macron akaibuka mshindi. 

Hata hivyo, Le Pen anasema wakati huu amejiandaa vema, hakikisho ambalo amelitoa wakati akizungumza na kituo cha Televisheni cha TF1. 

Kura za maoni zinaonesha kuwa, Macron atashinda kwa kupata asilimia kati ya 53 hadi 55 huku Le Pen akipata asilimia kati ya 44.5 hadi 47. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.