Pata taarifa kuu

Kansela wa Austria azungumzia kuhusu majadiliano "magumu" na Putin

Kansela wa Austria Karl Nehammer amepokelewa na Rais Vladimir Putin siku ya Jumatatu tarehe 11 Aprili. Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Ulaya tangu mwanzoni mwa uvamizi waUrusi nchini Ukraine, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na baraza wasaidizi wake baada ya mkutano huo.

Kansela wa Austria Karl Nehammer wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Vladimir Putin huko Moscow mnamo Jumatatu Aprili 11.
Kansela wa Austria Karl Nehammer wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Vladimir Putin huko Moscow mnamo Jumatatu Aprili 11. © REUTERS - MAXIM SHEMETOV
Matangazo ya kibiashara

Kansela wa Austria Karl Nehammer amesema "alikata tamaa" baada ya mkutano wake na Vladimir Putin, ambaye anataka kupata "ushindi wa kijeshi" nchini Ukraine. "Hatupaswi kuwa na udanganyifu wowote (...). Rais Putin ameingia kwa kiasi kikubwa katika mantiki ya vita na anafanya ipasavyo,” ametangaza mbele waandishi wa habari mwishoni mwa ziara yake.

"Mazungumzo na Rais Putin yalikuwa mazuri, ya wazi na magumu," Karl Nehammer ametangaza baada ya mkutano huo ambao ulichukua zaidi ya saa moja na wawili hao hawakusabahiana kwa kupeana mkono, kulingana na vyombo vya habari vya Austria. "Nilizungumza kuhusu uhalifu mkubwa wa kivita huko Bucha na maeneo mengine, nikisema kwamba wale wote waliohusika lazima wafikishwe mahakamani", ameongeza Kansela wa Austria.

Bucha, eneolililo  karibu na mji mkuu Kyiv, imekuwa ishara ya ukatili. Moscow imekataa kabisa kuhusika kwake katika mauaji hayo. "Nilimweleza Rais wa Urusi udharura wa kuweka maeneo ya usalama wa kiutu kwa kuezesha kuleta maji na chakula na kuwahamisha wanawake, watoto na waliojeruhiwa kutoka katika miji iliyozingirwa", amesisitiza Kansela huyo , akisisitiza kwamba "sio ziara ya kirafiki".

Mahojiano hayo yalifanyika katika makazi ya Novo-Ogaryovo karibu na Moscow. Hakuna picha iliyovuja kutoka kwa mkutano huo na hakuna mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari ambao umepangwa. Kulingana na msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, maazungumzo haya ya faragha yaliamuliwa kwa mpango wa upande wa Austria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.