Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Rais Zelensky ahofia makumi ya maelfu kuuawa huko Mariupol

Katika siku ya 47 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, luteka ya kijeshi inaendelea mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na hali ya ya kujiandaa kwa shambulio kubwa la Urusi katika mikoa ya Donetsk na Luhansk. Mwishoni mwa wiki hii, mashambulizi ya anga ya Urusi yaliendelea katika mikoa ya Kharkiv na Dnipro, wakati zoezi la kuhamisha raia ulikiendelea katika mikoa ya Donbass.

Huko Mariupol, raia walizikwa karibu na makazi yawatu.
Huko Mariupol, raia walizikwa karibu na makazi yawatu. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Ukraine limesema Jumatatu kuwa linajiandaa kwa "vita vya mwisho" katika mji uliozingirwa wa Mariupol, wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akikadiria kuwa makumi ya watu wanaweza kuwa wameuawa katika bandari ya bahari ya Azov.

Wakati huo huo Kansela wa Austria Karl Nehammer atakuwa kiongozi wa kwanza wa Ulaya kuzuru Moscow siku ya Jumatatu tangu kuanza kwa vita. Ujumbe ambao huenda ukakabiliana an hali ya hatari wakati Kyiv inajiandaa kwa mashambulizi makubwa ya Urusi huko Mashariki.

Benki ya Ufaransa ya Societe Generale imetangaza leo Jumatatu "kusitisha shughuli zake" nchini Urusi na itauza hisa zake zote katika kampuni ya Rosbank, kampuni kubwa katika sekta ya benki nchini Urusi, pamoja na matawi yake ya bima nchini humo.

Kulingana na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine Iryna Venediktova, miili 1,222 imepatikana katika mkoa wa Kyiv hadi sasa. Ripoti hii mpya, haielezei, hata hivyo, ikiwa miili iliyogunduliwa ilikuwa ya raia pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.