Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Jeshi lajiandaa kwa "vita vya mwisho" Mariupol

Ukraine inaendelea na luteka yake ya kijeshi mashariki mwa nchi hiyo, dhidi ya hali inayowezekana ya shambulio kubwa la Urusi katika mikoa ya Donetsk na Lugansk, wakati zoezi la kuhamisha raia linaendelea katika mikoa ya Donbass.

Ukumbi wa michezo wa Mariupol uliharibiwa kwa mashambulizi ya anga ya Urusi, Aprili 10, 2022.
Ukumbi wa michezo wa Mariupol uliharibiwa kwa mashambulizi ya anga ya Urusi, Aprili 10, 2022. REUTERS - STAFF
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Ukraine limesema Jumatatu kuwa linajiandaa kwa "vita vya mwisho" katika mji uliozingirwa wa Mariupol, wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akikadiria kuwa makumi ya watu wanaweza kuwa wameuawa katika bandari ya bahari ya Azov.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenkskiy ameendeleza kampeni yake ya kutafuta uungwaji mkono wa kimataifa huku akionya kwamba wiki zijazo huenda zikawa muhimu. Katika ujumbe wake kwa njia ya video usiku wa kuamkia leo, Rais huyo wa Ukraine amesema Urusi itaogopa zaidi na kwamba itakuwa na hofu ya kushindwa katika vita hivyo.

Siku ya Ijumaa, Ukraine ilidai kuwa takriban wanajeshi 19,000 wa Urusi wameuawa katika mapigano hayo. Mnamo Machi 25, Urusi iliweka idadi yake ya wanajeshi waliouawa kuwa 1,351.

Kwa upande mwingine Kituo cha Telegram cha Belarusi Belaruski Hayun, kinachounga mkono Ukraine kinasema kuwa kimeona harakati kubwa za usafirishaji wa vifaa vya jeshi la Urusi kwa treni kote Belarus siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.