Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Volodymyr Zelensky atoa wito wa kuongezwa kwa silaha zinazotolewa

Katika siku ya 45 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Aprili hii 9, ni hasira ambayo inatawala baada ya shambulio lililohusishwa na Urusi siku ya Ijumaa ya kituo cha Kramatorsk, katika Donbass, ambayo ilisababisha vifo vya hamsini, ikiwa ni pamoja na watoto watano.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. AP
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameanza ziara ya kushtukiza katika mji wa Kyiv Jumamosi (Aprili 9), na kumfanya kuwa kiongozi wa kwanza wa G7 kuzuru Ukraine tangu Urusi ilipoanza uvamizi wake dhidi ya Ukraine mnamo Februari 24. Boris Johnson ameahidi kuipatia Ukraine magari ya kivita na makombora ya kukinga meli na kutoa wito kwa nchi nyingine "kuiga mfano wa Uingereza".

Takriban euro bilioni 10 zimekusanywa wakati wa harambee ya kimataifa ya kuunga mkono Ukraine. Miongoni mwa euro bilioni zilizotolewa na Tume ya Ulaya, "milioni 600 zitaenda kwa mamlaka ya Ukraine na sehemu kwa Umoja wa Mataifa", amebainisha Ursula von der Leyen, ambaye anathibitisha kwamba euro milioni 400 zitalipwa kwa Marekani katika mstari wa mbelekatika mapokezi ya wakimbizi.

Takriban watu 52 waliuawa na 109 kujeruhiwa katika shambulio la roketi kwenye kituo cha reni cha Kramatorsk huko Donbass, ambapo raia wanakimbilia kutoroka eneo hili la mashariki mwa Ukraine. Moscow imekanusha kuhusika na shmbulizi hilo na kushutumu "uchochezi" wa vikosi vya Kyiv. Uokoaji umeendelea Jumamosi hii kwa njia ya barabara.

Mamlaka za itaa bado inajaribu kuwahamisha raia. Viwanja kumi vya kutoa misaada ya kibinadamu vilitakiwa kuanzishwa siku ya Jumamosi ili kuwahamisha raia katika mikoa ya kusini mashariki mwa nchi ambako mapigano sasa yamekithiri, alitangaza Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.