Pata taarifa kuu

Urusi yawafukuza wanadiplomasia 45 wa Poland kwa kujibu hatua iliyochukuliwa na Warsaw

Urusi imetangaza siku ya Ijumaa kuwafukuza wanadiplomasia 45 wa Poland kwa kulipiza kisasi kwa hatua iliyochukuliwa na Warsaw mwishoni mwa mwezi Machi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Rais wa Urusi Vladimir Putin. © SPUTNIK / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Kwa sababu ya kanuni ya usawa, wafanyakazi 45 wa ubalozi wa Poland na balozi zake ndogo huko Irkutsk, Kaliningrad na Saint Petersburg wametangazwa kuwa 'wamepoteza imani'," kwa serikali ya Urusi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema katika taarifa.

Wanadiplomasia hawa watalazimika kuondoka Urusi ifikapo Aprili 13, kulingana na chanzo hicho.

Poland ilitangaza mwishoni mwa mwezi Machi kuwafukuza "majasusi 45 wa Urusi wanaojifanya wanadiplomasia", katika muktadha wa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yaliyotekelezwa tangu Februari 24.

Hatua hii inaonyesha "nia ya Warszawa kuharibu kabisa mahusiano ya nchi mbili", imeshutumu diplomasia ya Urusi siku ya Ijumaa.

Katika siku za hivi karibuni, makumi ya wanadiplomasia wa Urusi wamefukuzwa kutoka nchi za Ulaya, zikiwemo Ujerumani, Italia, Ufaransa na Uhispania. Moscow inapaswa kujibu.

Siku ya Ijumaa, Urusi imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wawili wa Bulgaria kufuatia hatua kama hiyo iliyochukuliwa mwezi Machi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.