Pata taarifa kuu

Ukraine: Urusi yaendelea kushushiwa lawama kwa mauaji ya halaiki Bucha

Jumuiya ya Kimataifa imeendelea kulaani mauaji ya raia katika mji wa Bucha nchini Ukraine yanayodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Urusi. 

Miili ya watu uliyookotwa huko Bucha, baada ya jeshi la Urusi kuondoka, Aprili 4, 2022.
Miili ya watu uliyookotwa huko Bucha, baada ya jeshi la Urusi kuondoka, Aprili 4, 2022. REUTERS - MARKO DJURICA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara nyingine, rais wa Marekani Joe Biden amemwita mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin kama mbabe wa kivita. 

Hata hivyo, Urusi imeendelea kukanusha madai ya wanajeshi wake kuhusika. 

Rais Volodymyr Zelenskyy ambaye atahotubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataufa hivi leo, ametembelea mji wa Bucha na kuufanaNisha kama eneo la makaburi ya halaiki.

Wakati huo huo Jeshi la Ukraine limesema wanajeshi wa Urusi wanajiandaa kufanya mashambulizi kusini mashariki mwa Ukraine. Mkuu wa jeshi la Ukraine amesema wanajeshi wa Urusi wanalenga kuikamata miji ya Popasna na Rubizhne katika majimbo ya Donetsk na Luhansk na mji wa bandari wa Bahari Nyeusi wa Mariupol.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.