Pata taarifa kuu

Bei ya mafuta yaongezeka duniani kufuatia vita inayoendelea Ukraine

Bei ya dunia kwa sasa kwa dumu moja la mafuta, imefikia dola 10 za marekani, na hii iliongezeka kuanzia mwezi mmoja uliopita baada ya Urusi kuivamia Ukraine. 

 Nchini Kenya kwa mfano, lita moja ya mafuta ni kati ya dola 1.16 hadi dola 1.18.
Nchini Kenya kwa mfano, lita moja ya mafuta ni kati ya dola 1.16 hadi dola 1.18. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Mpaka kufikia Februari 24 mwaka huu, pipa moja la mafuta ghafi lilifikia dola za Marekani 100, ambapo sasa imefikia dola 105, hili likiwa ongezeko la juu zaidi kushuhudiwa tangu mwaka 2014. 

Nchini Kenya kwa mfano, lita moja ya mafuta ni kati ya dola 1.16 hadi dola 1.18, huku nchini Uganda, kwa sasa lita moja ya mafuta ya Petroli inauzwa shilingi elfu 5500 kwa mijini na zaidi ya elfu 7 katika maeneo ya mbali ambapo ni sawa na dola 1 hadi 2 za Marekani. 

Wataalamu wa masuala ya uchumi, wameonya kuhusu hali hii kuchangia bidhaa nyingine za kawaida kuongezeka bei, kutokana na shughuli za uendeshaji, athari hizi zikitarajiwa kuchukua muda ikiwa vita ya Ukraine haitamalizika
Wataalamu wa masuala ya uchumi, wameonya kuhusu hali hii kuchangia bidhaa nyingine za kawaida kuongezeka bei, kutokana na shughuli za uendeshaji, athari hizi zikitarajiwa kuchukua muda ikiwa vita ya Ukraine haitamalizika RFI / Olivier Rogez

 Nchini Tanzania, lita moja ya Petroli imefikia kati ya dola 1 hadi dola 1.11 za Marekani, bei hizi zikifanana kwa karibu za zile za nchini Rwanda, huku nchini Burundi lita moja ikiuzwa kwa hadi dola 1.34. 

 Wataalamu wa masuala ya uchumi, wameonya kuhusu hali hii kuchangia bidhaa nyingine za kawaida kuongezeka bei, kutokana na shughuli za uendeshaji, athari hizi zikitarajiwa kuchukua muda ikiwa vita ya Ukraine haitamalizika. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.