Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Urusi yakanusha kuhusika katika 'uhalifu wa kivita' huko Bucha

Nchini Ukraine, wakati huu wanajeshi wa Urusi wakiondoka katika maeneo yanayokaribia jiji kuu la Kyiv, imebainika kuwa wametekeleza mauaji ya raia katika mji wa Bucha. 

Wanajeshi wa Ukraine wakitembea kati ya vifaru vya Urusi vilivyoharibiwa kwenye mji wa Bucha ambapo miili ya zaidi ya raia 400 ilipatikana baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi.
Wanajeshi wa Ukraine wakitembea kati ya vifaru vya Urusi vilivyoharibiwa kwenye mji wa Bucha ambapo miili ya zaidi ya raia 400 ilipatikana baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi. AP - Rodrigo Abd
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa dunia wakiongozwa na rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron wamelaani mauaji ya raia zaidia ya 20 ambayo miili yao imeonekana katika barabara za mji huo. 

Hata hivyo, Urusi imekanusha madai ya kuhusika na mauaji hayo, wakati huu Umoja wa Mataifa ukisema watu 1400 wameuawa na wengine 2,000 wamejeruhiwa katika vita vinavyoendelea nchini Ukraine. 

Ukraine siku ya Jumapili iliishutumu Urusi kwa kufanya "mauaji ya halaiki", siku moja baada ya kugunduliwa kwa miili mingi ya raia katika mji wa Bucha, karibu na mji wa Kyiv, baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Moscow, jambo ambalo lilizua hasira Ulaya na Marekani.

Urusi imekanusha kuhusika katika kile inachokichukulia kuwa chokochoko za Ukraine na imeomba mjadala katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.