Pata taarifa kuu

Macron: Urusi ‘italazimika kujibu kuhusu makosa inayodaiwa kuyatenda’ Boutcha

Katika siku ya 39 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumapili hii Aprili 3, wakati Ukraine ikitangaza kuwa imelikomboa kabisa eneo la kyiv, milio ya mizinga imechukuwa na fasi ya kutoa heshima kwa maiti za raia zilizozagaa mitaani katika baadhi ya miji iliyoharibiwa.

Moscow imeondoa vikosi vyake vingi katika siku za hivi karibuni
katika mikoa ya kyiv na Chernigiv (kwenye picha), kaskazini mwa Ukraine.
Moscow imeondoa vikosi vyake vingi katika siku za hivi karibuni katika mikoa ya kyiv na Chernigiv (kwenye picha), kaskazini mwa Ukraine. REUTERS - SERHII NUZHNENKO
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► MashambulizI mbalimbali yamelenga miundombinu katika bandari ya Odessa Jumapili asubuhi.

► Baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi karibu na Kyiv, Waukraine wamerudi katika miji yao iliyoharibiwa kwa kiasi na maiti nyingi za raia zikiwa zimetapakaa mitaani, kama huko Boutcha. Baadhi ya watu walikuwa wamefungwa mikono walipouawa. Charles Michel, mkuu wa Umoja wa Ulaya ameshutumu "ukatili" na kutoa wito wa vikwazo vipya.

► Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa Jumapili hii huko Moscow ambapo atajaribu kupata hakikisho la "usitishwaji mapigano" nchini Ukraine.

► Mpatanishi mkuu wa Urusi siku ya Jumapili alighadhabishwa na matamshi ya mwenzake wa Ukraine ambaye alikuwa amebaini Jumamosi jioni kwamba Moscow ilikuwa imekubali "kwa maneno" mapendekezo makuu ya Ukraine.

Marekani na NATO zimeelezea kusikitishwa na ripoti za ukatili dhidi ya raia vitendo vinavyodaiwa kutekelezwa na vikosi vya Urusi huko Boutcha, na kuonya kwamba kuondoka kwa Moscow katika eneo hilo haimaanishi 'kujiondoa halisi' wala matumaini ya kupungua kwa uhasama.

Jeshi la Urusi limehamia mbali na viunga vya Kyiv lakini halijaondoka kaskazini mwa Ukraine na hali hiyo inaweza kusababisha mashambulizi mapya, amesema Jens Stoltenberg, katibu mkuu wa NATO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.