Pata taarifa kuu

Urusi 'yaondoa haraka' wanajeshi wake Kaskazini mwa Ukraine

Vikosi vya Urusi vimeanza kuondoka katika mikoa ya Kyiv na Cherniguiv kaskazini mwa Ukraine, na vinalenga "kupata kuweka nguvu zaidi mashariki na kusini", mshauri wa rais wa Ukraine amesema Jumamosi.

Wanajeshi wa Ukraine wakikagua mitaro iliyotumiwa na askari wa Urusi wakati wa uvamizi wa vijiji karibu na Kyiv mnamo Aprili 1.
Wanajeshi wa Ukraine wakikagua mitaro iliyotumiwa na askari wa Urusi wakati wa uvamizi wa vijiji karibu na Kyiv mnamo Aprili 1. AP - Rodrigo Abd
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewaonya raia wake kuwa wanajeshi wa Urusi wanaoondoka katika maeneo yao na wanatengeneza kile ametaja ni "mazingira ya maafa" nje ya mji mkuu kwa kutega mabomu ya ardhini katika eneo zima hata karibu na nyumba za watu na maiti.

Hayo yanajiri wakati mzozo wa kiutu katika mji uliozingirwa wa Mariupol unaendelea kutokoto. Wanajeshi wa Urusi walizuia operesheni za kuwahamisha watu kwa siku ya pili mfululizo siku y Ijumaa.

Katika hatua nyingine zaidi ya watu 3,000 "wameokolewa" kutoka Mariupol, mji wa kusini mashariki mwa Ukraine uliozingirwa na vikosi vya Urusi, alisema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika video iliyotolewa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi.

Hayo ya kijiri Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Kibinadamu, Martin Griffiths, atakuwa mjini Moscow siku ya Jumapili kujaribu kuomba "usitishwaji mapigano kwa kuokoa maisha ya raia" nchini Ukraine, mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alitangaza siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.