Pata taarifa kuu

Mwendesha mashtaka: Miili ya raia 410 yapatikana karibu na Kyiv

Katika siku ya 39 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumapili hii Aprili 3, wakati Ukraine ikitangaza kuwa imelikomboa kabisa eneo la kyiv, milio ya mizinga imechukuwa na fasi ya kutoa heshima kwa maiti za raia zilizozagaa mitaani katika baadhi ya miji iliyoharibiwa.

Wafanyakazi wa manispaa wakibeba mifuko ya miili ya watu katika mji wa Bucha, karibu na mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, Aprili 3, 2022.
Wafanyakazi wa manispaa wakibeba mifuko ya miili ya watu katika mji wa Bucha, karibu na mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, Aprili 3, 2022. AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Ukraine imeishutumu Urusi kwa kufanya "mauaji ya halaiki", siku moja baada ya kugunduliwa kwa miili mingi ya raia katika mji wa Bucha, karibu na Kyiv, baada ya kuondolewa kwa wanajeshi wa Moscow katika mji huo, hali ambayo imezua hasira Ulaya na Marekani.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg amese,a vifo vya raia katika mji wa Bucha "havikubaliki".

Akizungumza na CNN, alisema vifo hivyo ni "ukatili dhidi ya raia ambao hatujaona Ulaya kwa miongo kadhaa" na kwamba "hii inasisitiza umuhimu wa vita hivi kukomeshwa".

Stoltenberg anaungana na viongozi wengine dunia kulaani matukio katika maeneo yaliyoachwa nyuma na majeshi ya Urusi waliondoka miji kadhaa inayozunguka Kyiv.

Kufuatia kujiondoa kwa Urusi kutoka Bucha, kumekuwa na ripoti nyingi za maiti zilizopatikana zimevaa nguo za kiraia.

Mpatanishi mkuu wa Urusi siku ya Jumapili ameghadhabishwa na matamshi ya mwenzake wa Ukraine ambaye alikuwa amebaini Jumamosi jioni kwamba Moscow ilikuwa imekubali "kwa maneno" mapendekezo makuu ya Ukraine.

Marekani na NATO zimeelezea kusikitishwa na ripoti za ukatili dhidi ya raia vitendo vinavyodaiwa kutekelezwa na vikosi vya Urusi huko Bucha, na kuonya kwamba kuondoka kwa Moscow katika eneo hilo haimaanishi 'kujiondoa halisi' wala matumaini ya kupungua kwa uhasama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.