Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Uchaguzi Ufaransa : Macron ataka kuwepo kwa ushawishi wa pamoja

Macron ambaye siku ya Jumamosi anatarajiwa kuhutubia umma kwa mara ya kwanza katika kampeni ya kutaka kuchaguliwa tena, ameomba kuwepo kwa ushawishi wa pamoja kutokana na wazo kuwa bado ushindi haujapatikana . 

Macron aliingia rasmi kwenye kampeni dakika za mwisho, akiashiria juhudi zake za kidiplomasia za kukomesha vita vinayoendelea nchini Ukraine.
Macron aliingia rasmi kwenye kampeni dakika za mwisho, akiashiria juhudi zake za kidiplomasia za kukomesha vita vinayoendelea nchini Ukraine. AP - Thibault Camus
Matangazo ya kibiashara

Uwepo wake katika mkutano huo ulikuja baada ya msururu wa kura za maoni kuonyesha mgombea wa mrengo wa kulia Marine Le pen anamkaribia sana, licha ya kuongoza katika kura za maoni za hapo awali. 

Kura ya maoni iliyochapishwa Jumatano na kampuni ya Elabe, inaonyesha Le Pen atapata  asilimia 47.5 katika duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya Macron ambaye angeshinda kwa asilimia 52.5. 

Macron aliingia rasmi kwenye kampeni dakika za mwisho, akiashiria juhudi zake za kidiplomasia za kukomesha vita vinayoendelea nchini Ukraine, wakati Le Pen alikuwa akiendelea na kampeni nchini humo kwa miezi kadhaa akiahidi kuimarisha uchumi wakati huu wa mfumuko wa bei. 

Wakati hayo yakijiri, raia Macron ameshtumiwa baada ya serikali yake kutumia fedha za umma kwa ajili ya kampuni za kibinfasi nchini Marekani McKinsey, kumsaidia katika masuala ya uongozi wake, wakati huu kura za maoni zikionesha kuwa, wapinzani wake hasa mwanasiasa wa mrengo wa kushoto Marine Le Pen, anamkaribia. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.