Pata taarifa kuu

White House: Biden atazuru Poland siku ya Ijumaa kuzungumza kuhusu Ukraine

Rais wa Marekani Joe Biden atafanya ziara kuelekea Warsaw siku ya Ijumaa kukutana na mwenzake wa Poland Andrzej Duda kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, Ikulu ya Marekani ilitangaza Jumapili.

Rais Joe Biden anaondoka baada ya kuzungumza kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine katika Chumba cha Mashariki cha Ikulu ya White House, Alhamisi, Februari 24, 2022, mjini Washington.
Rais Joe Biden anaondoka baada ya kuzungumza kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine katika Chumba cha Mashariki cha Ikulu ya White House, Alhamisi, Februari 24, 2022, mjini Washington. AP - Alex Brandon
Matangazo ya kibiashara

"Rais atajadili jinsi Marekani, pamoja na washirika wetu na marafiki zetu, watakabiliana na mzozo wa kibinadamu na haki za binadamu ambao vita vya Urusi visivyo na msingi vimesababisha" , msemaji wa White House Jen Psaki alisema katika taarifa kutoka Ikulu ya Marekani.

Taarifa inaongeza kuwa ziara hiyo ya Joe Biden itafanyika baada ya ziara yake nchini Ubelgiji kukutana na viongozi wa NATO, G7 na Umoja wa Ulaya. "Safari hii italenga kuendelea kuhamasisha ulimwengu kuwaunga mkono raia wa Ukraine na kupinga uvamizi wa Rais Putin nchini Ukraine," alisema. "Lakini hakuna mipango ya kwenda Ukraine," alisema Jen Psaki.

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki, akifuatana na viongozi wenzake wa Czech na Slovenia, walisafiri hadi Kyiv wiki iliyopita huku mji mkuu wa Ukraine ukiwa umezingirwa kufuatia uvamizi wa Urusi Februari 24 nchini humo.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alikuwa tayari amekutana na Andrzej Duda mjini Warsaw mapema mwezi Machi, wote wakilaani hatua ya kijeshi ya Urusi, hasa dhidi ya raia. Mazungumzo hayo yalifanyika muda mfupi baada ya Washington kukataa ombi la Poland la kutuma ndege za kivita aina ya MiG-29 kwenda Ukraine kupitia kituo cha anga cha Marekani. Kwa upande wa Marekani, pendekezo hili liliibua "wasiwasi mkubwa" kwa Muungano mzima wa Atlantic.

Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa karibu watu milioni 10 wa Ukraine wamekimbia makazi yao, ambao karibu theluthi moja wamekwenda nje ya nchi, hasa Poland.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.