Pata taarifa kuu

Ukraine: Watu milioni kumi wamekimbia makazi yao, kulingana na Filippo Grandi

"Vita nchini Ukraine ni mbaya sana na kwamba watu milioni 10 wamekimbia, ama wakimbizi wa ndani au wakimbizi walio nje ya nchi," Bwana Grandi, Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi, UNHCR, amesema kwenye Twitter.

Filippo Grandi amesema watu milioni 10, ikiwa ni zaidi ya robo ya idadi jumla ya raia wa taifa hilo wameikimbia Ukraine kutokana kile alichokiita vita vya maangamizi vya Urusi.
Filippo Grandi amesema watu milioni 10, ikiwa ni zaidi ya robo ya idadi jumla ya raia wa taifa hilo wameikimbia Ukraine kutokana kile alichokiita vita vya maangamizi vya Urusi. AP - SALVATORE DI NOLFI
Matangazo ya kibiashara

UNHCR imebaini kwamba watu 3,389,044 wameondoka nchini Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mnamo Februari 24, na kwamba wengine 60,352 wako njiani kuelekea nje ya nchi. Wanawake na watoto, ni miongoni mwa wakimbizi hao. Wanaume walio kati ya umri wa miaka 18 na 60 wamekataliwa kuondoka na kwa wakati wowote wanaweza kuitwa kutetea taifa lao.

Filippo Grandi amesema watu milioni 10, ikiwa ni zaidi ya robo ya idadi jumla ya raia wa taifa hilo wameikimbia Ukraine kutokana kile alichokiita vita vya maangamizi vya Urusi.

Wakati huo huo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF,  limesema watoto milioni 1.5 ni miongoni mwa waliokimbilia uhamishoni, na kuonya hatari ya kukabiliwa na biashara haramu ya usafirishaji watu na utumikishwaji mbaya.

Kabla ya mgogoro huu wa sasa Ukraine ilikuwa na jumla ya watu milioni 37. Idadi hiyo inajumushia maeneo yaliokuwa katika udhibiti wa serikali ukiliondoa eneo lililonyakuliwa na Urusi la Crimea na maeneo ya wanaotaka kujitenga yenye kuunga mkono Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.