Pata taarifa kuu

Ukraine yakataa kusalimu amri mbele ya Urusi

Ukraine imekataa agizo la Urusi, kuwa vikosi vyake vijisalimishe na kuweka silaha chini kwenye mji wa Mariupol ambao umeendelea kushuhduia mashambulizi mazito.

Wanajeshi wa Urusi wamekataa kuweka chini silaha, baada ya kuombwa na Urusi kufanya hivyo.
Wanajeshi wa Urusi wamekataa kuweka chini silaha, baada ya kuombwa na Urusi kufanya hivyo. AFP - BULENT KILIC
Matangazo ya kibiashara

Urusi ilikuwa imeviambia vikosi vya Ukraine viondoke kwenye mji huo wa Pwani, kufikia saa 11 Alfajiri, siku ya Jumatatu, saa za Moscow, lakini Kiev imesema hilo haliwezekani.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilidokeza kuwa, iwapo wanajeshi wa Ukraine wangejisalimisha, mipango ingewekwa ili kuwaruhusu watu kuondoka katika mji huo ambao kwa wiki kadhaa sasa umegeuka kuwa uwanja wa mapambano.

Wakati hayo yakijiri, Meya wa mji wa Chernigiv, Kaskazini mwa Ukraine amesema raia kadhaa wamepoteza maisha bdaada ya vikosi vya Urusi kushambulia hospital moja.

Naye rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwahotubia wabunge wa Israel ameendeleza wito wake wa mazunngumzo na Urusi ili kusitisha vita vinavyoendelea huku akisema mji wa Jerusalem, ni êneo sahihi la kuandaa mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.