Pata taarifa kuu

Mzozo wa Ukraine: Boris Johnson amtaka Vladimir Putin kutothubutu kuivamia Ukraine

Viongozi wa nchi za Magharibi wanaendelea kuiomba Moscow kutuliza hali nchini Ukraine. Jumatatu hii, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa wito kwa Vladimir Putin kuondoa wanajeshi wake karibu na mpaka na Ukraine.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anawasili Ukraine katika kuonyesha uungwaji wake mkono kwa Keiv.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anawasili Ukraine katika kuonyesha uungwaji wake mkono kwa Keiv. JESSICA TAYLOR UK PARLIAMENT/AFP
Matangazo ya kibiashara

BoJo amebaini kwamba hali ni "hatari sana" na kuna uwezekano wa uvamizi wa Urusi "ndani ya saa 48 zijazo". "Tunatoa wito kwa kila upande kufanya mazungumzo (...) ili kuepuka kosa ambalo litakuwa janga," ameongeza. Boris Johnson ameamua kukatiza ziara yake huko Kaskazini Magharibi mwa Uingereza ili kurejea London, "kulingana na hali ilivyo sasa", amesema msemaji.

Baada ya Uingereza kuwashauri raia wake siku ya Ijumaa kuondoka Ukraine mara moja, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss alikuwa anatarajiwa kuongoza mkutano wa kujadili jinsi ya kuondokana na mgogoro huo siku ya Jumatatu alasiri kuhusu jibu la kuhusiana na hali ya sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.