Pata taarifa kuu

Ukraine yaashiria wasiwasi wa Magharibi juu ya nia ya Moscow

Katika siku za hivi karibuni, jumbe zinazozidi kutia wasiwasi zimekuwa zikitoka Washington, huku baadhi ya vyanzo vya kijasusi vikipendekeza uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine mapema wiki ijayo au angalau kabla ya kumalizika kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi huko Beijing.

Waziri wa Mmbo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Februari 12, 2022.
Waziri wa Mmbo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Februari 12, 2022. AP - Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

"Kwa sasa, rafiki mkubwa wa adui zetu ni hofu katika nchi yetu. Na taarifa hizi zote husababisha tu hofu na hazitusaidii”, amelaani Jumamosi Volodymyr Zelensky, aliyenukuliwa na shirika a habari la  Interfax-Ukraine. Wakati jumbe za kutatanisha, hasa kutoka Washington, zikifuatana, rais wa Ukraine ameamua kwamba kulikuwa na matangazo "mengi" yanayotangaza "vita vikali kwa upande wa Urusi". "Ikiwa mna taarifa zaidi kuhusu uvamizi wa uhakika wa 100%, tupeni! ", bado amesisitiza.

Wafanyakazi wasio wa lazima watakiwa kuondoka kwenye balozi zao

Urusi imeharakia kutangaza Jumamosi hii kwamba ubalozi wake mjini Kiev utaendelea kufanya kazi kama kawaida, tofauti na nchi mbalimbali kama vile Israel, Uingereza, Ujerumani, Uholanzi au Marekani ambazo zilitangaza kuwaondoa wanadiplomasia wao kutoka mji mkuu wa Ukraine.

 Hayo yanajiri wakati Ikulu ya White House ilisema siku ya Ijumaa kuwa uvamizi wa Urusi dhidi ay Ukraine unaweza kuanza na mlipuko wa angani ambao utafanya safari za angani kuwa ngumu na kuhatarisha raia, Ikulu ya Marekani ilisema Ijumaa.

Moscow imekanusha mara kwa mara mpango wowote wa kuivamia Ukraine licha ya kuwakusanya zaidi ya wanajeshi 100,000 karibu na mpaka.

"Uchochezi"

Kinyume chake, kumekuwa kukipigwa kelele tangu mwanzo wa mgogoro huu kwamba hapana, Urusi haina nia ya kuivamia Ukraine. Siku ya Jumamosi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov aliishutumu Marekani kwa "uchochezi" wakati wa mazungumzo ya simu na mwenzake wa Marekani Antony Blinken, kulingana na taarifa kutoka kwa wizara yake. Lakini Urusi bado inaongeza mazoezi ya kijeshi, hasa katika Bahari Nyeusi, na harakati za wanajeshi wake kuelekea Magharibi, wakati majadiliano na kambi ya Magharibi yamesimama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.