Pata taarifa kuu

Olaf Scholz akutana na Biden kuonyesha umoja wa nchi za Magharibi dhidi ya Urusi

Juhudi za kidiplomasia kujaribu kuzuia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine zinaendelea. Wakati Emmanuel Macron yuko nchini Ukraine, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz yuko Washington tangu siku ya Jumatatu kwa lengo la kuonyesha umoja wa nchi za Magharibi dhidi ya Urusi, lakini sio kazi rahisi.

Rais Joe Biden na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz wakisikiliza maswali kutoka kwa mwandishi wa habari wakati wa mkutano wa wanahabari katika Ikulu ya White House, Jumatatu, Februari 7, 2022, Washington.
Rais Joe Biden na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz wakisikiliza maswali kutoka kwa mwandishi wa habari wakati wa mkutano wa wanahabari katika Ikulu ya White House, Jumatatu, Februari 7, 2022, Washington. AP - Alex Brandon
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuanza kwa mgogoro huo, Marekani imeahidi vikwazo visivyo na kifani iwapo Urusi itaivamia Ukraine na kusisitiza juu ya umoja wa nci za Magharibi. Lakini Ujerumani inaona kwamba kauli hizi zinazidi kuchochea mvutano. Kiasi kwamba Joe Biden analazimika kusisitiza kuhusu imani yake kwa Olaf Scholz. “Hakuna haja ya kurejesha imani kati ya nchi hizi mbili. Ana imani kamili na Marekani. Ujerumani ni mojawapo ya washirika wetu muhimu zaidi duniani. Hakuna shaka kuhusu ushirikiano wa Ujerumani na Marekani. Hakuna, "alisisitiza rais wa Marekani.

Isipokuwa ni wazi kuwa kuna alama za kushikamana. Kwa mfano juu ya hatima ya bomba la gesi la Nord Stream 2 ambalo linaunganisha moja kwa moja Urusi na Ujerumani kupitia Bahari ya Baltic. Marekani imekuwa ikiipinga kwa muda mrefu na Joe Biden ametangaza kufungwa kwa bomba hilo iwapo kutatokea uvamizi. "Iwapo Urusi itavamia Ukraine, na vifaru au askari kuvuka mpaka wa Ukraine, basi hakutakuwa tena na bomba la Nord Stream 2. Tutakuwa tumemaliza. »

Olaf Scholz, wakati huo huo, ameoekana kuwa mwangalifu bila kutaja bomba la kusafirisha gesi kutoka Urusi kwenda Ujerumani la Nord Stream 2. “Tunachukuwa hatua pamoja. Tumeungana kabisa. Hatutachukua hatua tofauti. Tutachukua hatua sawa na zitakuwa ngumu sana kwa Urusi na wanapaswa kuelewa hilo. Olaf Scholz pia anakumbusha kuwa nchi yake ni mojawapo ya wachangiaji wakubwa wa misaada ya kiuchumi kwa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.