Putin aishtumu Marekani kwa kujaribu kuingiza urusi kwenye vita
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameishtumu Marekani kwa kuendelea kuichochea nchi yake kuingia kwenye vita na Ukraine, kwa kile alichokieleza Washington inatafuta mbinu za kuiwekea Moscow vikwazo.
Imechapishwa:
Aidha, ameilamu Marekani kwa kupuuza malalamishi yake ya kiusalama, iwapo Ukraine itaruhusiwa kuwa mwanachama wa Jeshi ya kujihami la nchi za Magharibi NATO.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Uingereza Bori Johnson ambaye amezuru Ukraine, amesema nchi yake na mataifa mengine ya Magharibi yako tayari kuichukulia Urusi hatua iwapo itaendelea na mpango wake.
Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa wakati huu, maelfu ya wanajeshi wa Urusi wakiendelea na mazoezi katika mpaka na Ukraine.