Pata taarifa kuu
UFARANSA-DIPLOMASIA

Mgogoro wa Ukraine: Emmanuel Macron kukutana kwa mazungumzo na Vladimir Putin

Siku chache kabla ya Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Emmanuel Macron anakwenda Moscow leo Jumatatu, Februari 7, kukutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. Mazungumzo yao yatagubikwa hasa na hali kuhusu Ukraine wakati hali hiyo inazidi kutokuwa na uhakika na uwezekano wa kudorora usalama kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kilele kuhusu Ukraine kwenye Ikulu ya Elysee mjini Paris mnamo Desemba 9, 2019.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kilele kuhusu Ukraine kwenye Ikulu ya Elysee mjini Paris mnamo Desemba 9, 2019. © Charles Platiau, AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wiki moja baada ya mazungumzo ya kwanza ya simu, huyu hapa Emmanuel Macron atakuwa na mazungumzo ya ana kwa ana huko Moscow na mwenzake wa Urusi Vladimir Poutine. Rais wa Ufaransa anatarajia kutafuta njia ya kupunguza mvutano kati ya Urusi na Ukraine.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atazuru jijini Moscow na Kiev kujaribu kutumia mbinu za kidiplomasia wakati huu kukiwa na wasiwasi kuwa Urusi huenda ikaivamia Ukraine

Macron atakuwa jijini Moscow leoJumatatu, kukutana na rais Vladimir Putin, na baadaye kukutana na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Jumanne jijini Kiev, huku Kansela Scholz akitarajiwa kuwa jijini Moscow Februari 15 na Kiev tarehe 14 Februari.

Ziara hii itakuja wakati huu Urusi ikiendelea kushinikiza kuhusu sharti lake la nchi jirani ya Ukraine kutoruhusiwa kujiunga na jeshi la nchi za Magharibi NATO kwa sababu za kiusalama.

Hivi karibuni, rais Macron alinzungumza kwa njia ya simu na viongozi hao wawili na kuafikiana kupata suluhu kwa njia ya mazungumzo.

Aidha, Urusi imeendelea kuyashtumu mataifa ya Magharibi ikiongozwa na Marekani kwa kuchochea uhuasiano wake na Ukraine na kuendelea kukanusha madai kuwa inapanga kuivamia Ukraine.

Marekani na washirika wake, wameendelea kuionya Urusi kuwa itachukuliwa hatua iwapo itaivamia Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.