Pata taarifa kuu

Jeshi la Urusi lazindua luteka katika Bahari Nyeusi, bandari zafungwa

Mazungumzo ya kidiplomasia yamekwama kati ya Ukraine na Urusi baada ya mkutano wa washauri wa marais wa Ukraine, Urusi, Ufaransa na Ujerumani, Alhamisi, Februari 10 huko Berlin, kama sehemu ya "muundo wa Normandy".

Meli kubwa ya Urusi "Admiral Essen" ikishiriki luteka katika Bahari Nyeusi, Januari 26, 2022.
Meli kubwa ya Urusi "Admiral Essen" ikishiriki luteka katika Bahari Nyeusi, Januari 26, 2022. via REUTERS - RUSSIAN DEFENCE MINISTRY
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa ofisi ya rais wa Ukraine, Andriy Yermak, alisema jana usiku kwamba mazungumzo hayo hayajapiga hatua yoyote, lakini pande hizo zitakutana tena wiki zijazo.

Wakati huo huo, shinikizo la kijeshi haliruhusu mipaka ya Ukraine kuwa wazi na shughuli zimesimama kwenye bandari za nchi hiyo, na wakati huu kwenye upande wa kusini, kwenye maji ya Bahari Nyeusi, vikosi vya wanamaji wa Urusi vimeanza mazoezi ya kijeshi.

Wakati huo huo Rais wa Marekani Joe Biden amewataka raia wa nchi yake wanaoishi nchini Ukraine, kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo, wakati huu Urusi ikidaiwa kuwa na mpango wa kuivamia nchi hiyo jirani. 

Biden amesema hali inaweza kubadilika wakati wowote, wakati huu, wanajeshi zaidi ya Laki Moja wa Urusi, wakiendelea na mazoezi katika mpaka na Ukraine. 

Licha ya wasiwasi huu, Urusi imekuwa ikikanusha mipango ya kutaka kuivamia Ukraine na kuishtumu Marekani kwa kuchochea mzozo huo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.