Pata taarifa kuu

Mgogoro Ukraine: Baada ya Moscow, Macron ziarani Kiev kujaribu kutuliza mvutano

Baada ya mazungumzo yake marefu na Vladimir Putin mjini Moscow Jumatatu jioni, Emmanuel Macron ameondoa na kwenda mjini Kiev, nchini Ukraine, kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Emmanuel Macron wakati wa ziara yake huko Moscow ambapo alikutana na Vladimir Putin mnamo Februari 7, 2022.
Emmanuel Macron wakati wa ziara yake huko Moscow ambapo alikutana na Vladimir Putin mnamo Februari 7, 2022. AP - Sergei Guneyev
Matangazo ya kibiashara

Rais wa nchi wa Ufaransa amependekeza kwa rais wa Urusi  kujenga dhamana thabiti ya usalama barani Ulaya, lakini pia atalazimika kuwatuliza nyoyo Waukraine, ambao wana wasiwasi sio tu juu ya kuongezeka kwa wanajeshi wa Urusi kwenye mipaka ya nchi hizo mbili, lakini pia kwa kujaribu kuendeleza mvutano.

Raia wa Ukraine ambao walifuatilia kwa karibu mkutano wa pamoja wa Emmanuel Macron na Vladimir Putin na waandishi wa habari Jumatatu usiku walishangazwa waliposikia rais wa Urusi akisema maneno yafuatayo kuhusu Ukraine: "Upende usipende, ndugu yangu, itabidi uuvumilie.." . Ukweli kwamba Vladimir Putin anatumia maneneo haya kusisitiza juu ya haja ya kutekelezwa kwa mikataba ya Minsk kunabainisha kwa raia wa Ukraine msimamo wa rais Putin katika uhusiano wake na Ukraine.

Wakati wakisubiri hotuba ya pamoja ya Emmanuel Macron na Volodymyr Zelensky, waangalizi wengi wa Ukraine wanahofia kwamba rais wa Ufaransa amekuja Kiev na madai mengi ya maelewano muhimu. Jumanne hii asubuhi, wachambuzi kadhaa wa Ukraine wamemlinganisha Emmanuel Macron na Neville Chamberlain, Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye alitia saini mikataba ya Munich mwaka 1938 na Ujerumani, ambayo haikuzuia vita.

Huko Kiev, wanaona kwamwa kimaadili sio sahihi kuomba maelewano zaidi kutoka kwa mshambuliwa kuliko kutoka kwa mchokozi.

Ukraine haitaki makubaliano yoyote juu ya uhuru

Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni Rais Volodymyr Zelensky alikuwa ametuma ishara kadhaa zinazopendekeza kwamba anaunga mkono mbinu ya upatanishi ya Emmanuel Macron. Kinyume na jumbe za kutisha kutoka Ikulu ya White House, serikali ya Ukraine ilisisitiza juu ya ukweli kwamba uvamizi wa Urusi haukukaribia kana kwamba Volodymyr Zelensky alitaka kuepusha hali yoyote ya hofu ambayo inaweza kuyumbisha nchi, na hasa uchumi wake.

Hata hivyo, kuna mistari nyekundu, iliyokumbushwa Jumatatu na Waziri wa Mambo ya Nje, Dmytro Kuleba: "suluhisho za kidiplomasia, ndiyo, lakini hakuna makubaliano juu ya uhuru", alitangaza. Kulingana na waziri huyo, raia wa Ukraine pekeendio wana haki ya kufafanua mwelekeo wa sera zao za kigeni.

Vladimir Putin na Emmanuel Macron pia wameahidi kukutana tena kwa mazungumzo hivi karibuni na rais wa Ufaransa ameamua kuwa siku chache zijazo zitakuwa za "maamuzi". Kulingana na Rais Macron, hakuna "suluhisho la kudumu ambalo halipitii diplomasia". Kwa hivyo anakuja Kiev kujaribu kuendelea na mpango wake wa kupendelea mazungumzo na kupunguza mvutano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.