Pata taarifa kuu

Mgogoro wa Ukraine: NATO yataka kuimarisha jeshi lake Mashariki

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson yuko katika makao makuu ya NATO huko Brussels Alhamisi, Februari 10. Alitangaza kuimarishwa kwa uwepo wa jeshi la Uingereza katika kikosi cha Muungano wa Atlantiki dhidi ya Urusi. Nchi nyingine kama vile Marekani, Denmark au Ufaransa, kwa mfano, tayari zimetoa matangazo kama hayo na, kwa upande wa Katibu Mkuu wa NATO amesema, "wakati huu ni hatari kwa usalama wa Ulaya".

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg katika makao makuu ya NATO huko Brussels mnamo Februari 10, 2022.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg katika makao makuu ya NATO huko Brussels mnamo Februari 10, 2022. AP - Olivier Matthys
Matangazo ya kibiashara

NATO - Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini - ni muungano wa kijeshi ulioundwa mwaka 1949 na nchi 12, ikiwemo Marekani, Canada, Uingereza na Ufaransa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, idadi ya wanajeshi wa Urusi nchini Belarus na Urusi inaongezeka na muda wa onyo wa kutokea mashambulizi unapungua. Wote yeye na Boris Johnson wanasema wakati huu ni hatari; Waziri Mkuu wa Uingereza ameibua uwezekano wa "janga", kama ilivyoripotiwa na mwandishi wetu wa habari huko Brussels, Pierre Benazet.

Kwa upande wa Muungano wa Atlantiki, wanaendelea kuzungumzia uimarishaji wa wanajeshi katika ukanda wa Mashariki. "Kwanza, tayari tumeongeza uwepo wetu katika sehemu ya mashariki ya Muungano," amesema Jens Stoltenberg. Pili, tumeongeza kiwango cha tahadhari ya askari ili waweze kuimarisha haraka ikiwa ni lazima. Na tatu, sisi pia kwa sasa tunasoma hitaji la mabadiliko ya muda mrefu katika mkao wetu katika sehemu ya mashariki ya Muungano. Leo tuna maeneo ya mapigano katika nchi za Baltic na Poland, lakini sasa tunazingatia kuwa na maeneo sawa ya mapigano katika eneo la Bahari Nyeusi, kwa mfano huko Rumania. »

Uimarishaji huu wa muda mrefu utakuwa mezani katika mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO siku ya Jumatano na Alhamisi. I

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aliwapokea viongozi wa nchi za Baltic jioni hii mjini Berlin

Wkati huo huo vikosi vya Urusi vimeanzisha luteka ya pamoja ya kijeshi ya siku kumi nchini Belarus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.