Pata taarifa kuu

Boris Johnson : Kamwe sintojiuzulu kwenye wadhifa wangu

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameendelea kupata shinikizo za kujiuzulu kutoka kwa wabunge kufuatia ripoti za kuandaa na kuhudhuria sherehe wakati mikusanyiko ya watu ilipokuwa imezuiwa kwa sababu ya janga la Covid-19.

BRITAIN-POLITICS/PMQS
BRITAIN-POLITICS/PMQS via REUTERS - UK PARLIAMENT/JESSICA TAYLOR
Matangazo ya kibiashara

Johnson ana wakati mgumu kumaliza mtafaruku uliozuka hata ndani ya chama chake ambapo baadhi ya wabunge walioghadhabishwa na sherehe hizo wanamtaka aachie ngazi

Mmoja wa wabunge wa chama chake cha Conservative, Christian Wakeford, amehamia chama kikuu cha upinzani cha Labour, huku Boris akijitetea mbele ya wabunge.

Uingereza kulegeza hatua kadhaadhidi ya Covid

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Uingereza amesema kuwa watu nchini humo hawatohitajika kuvaa barakoa mahali popote au kufanyia kazi nyumbani kuanzia wiki ijayo. Johnson amesema wanasayansi wanaamini kwamba wimbi la kirusi cha Omicron limesambaa kote nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.