Pata taarifa kuu
UINGEREZA-SIASA

Uingereza: Waziri Mkuu Boris Johnson kuachia ngazi kufuatia sakata linaloendelea

Vyombo vya habari nchini Uingereza vinaendelea kuzungumzia kuhusu uwezekano wa mtu mwingine kuchukuwa nafasi ya Waziri Mkuu wa sasa nchini humo Boris Johnson, baada ya mvutano uliozuka kufuatia kukiuka kwaKe kwa sheria za kudhibiti ugonjwa wa Covid-19.

Waziri Mkuu Boris Johnson wakati alipozuru kituo cha chanjo huko Northampton, Januari 6, 2022.
Waziri Mkuu Boris Johnson wakati alipozuru kituo cha chanjo huko Northampton, Januari 6, 2022. Peter Cziborra Pool/AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Katika vyombo vya habari vya Uingereza, tayari kuna uvumi kuhusu enzi ya baada ya Boris.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimekuwa vikizungumza juu ya Boris Johnson kupoteza imani yake kwa muda sasa. Swali sasa ni lini na vipi atafukuzwa kazi, kwa kura ya kutokuwa na imani naye - kwa mfano - ambayo itafanya kujiuzulu kwake kuwa moja kwa moja, kulingana na mwandishi wetu wa London, Sidonie Gaucher.

Hata kutoka kwenye chama chake, baadhi ya wabunge na maseneta nao wanamtaka aondoke serikalini. Kwa hivyo Boris Johnson anaweza kulazimishwa kujiuzulu, shinikizo kutoka kwa chama chake na kutoka kwa serikali ikiwa kura za kutosha zitakusanywa kati ya walio wengi. Kwa mujibu wa Sophie Loussouarn, daktari aliyebobea katika historia ya kisiasa ya Uingereza, hatakuwa habari njema kwa walio wengi pia: "Kujiuzulu huku sio sawa, kwa sababu katikati ya mgogoro wa kiafya, haitakuwa sahihi kufanyika kwa uchaguzi kwa uongozi wa Chama cha Conservative. Kila kitu kitategemea na msimamo wa wabunge wa kutoka cha Conservative. »

Rishi Sunak na Liz Truss, kuchukua nafasi ya Boris JohnsonMajina ya watu kadhaa wanaoshukiwa kuchukuwa mikoba ya Boris Johnson yameanza kutajwa. Kwanza, kuna Rishi Sunak, Chancellor of the Exchequer, yaani Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Hazina? ambaye aliteuliwa kwenye nafasi hiyo FebruarI 13, 2020. Mtetezi huyu wa Brexit aliye na mtindo wa kipekee ndiye wa kwanza kwenye orodha. Kisha, Liz Truss pia ametajwa. Waziri wa Mambo ya Nje anasifika kwa uwazi wake. Bingwa wa biashara huria, alifikia mfululizo wa mikataba ya biashara baada ya Brexit.

Pia anatajwa Dominic Raab, Waziri wa Sheria wa sasa ambaye alichukuwa nafasi ya Boris Johnson alipoambukizwa virusi vya Corona. Michael Gove, Waziri wa Makazi wa sasa ambaye dhamira yake ni "kuinua" maeneo yenye hali duni ya Uingereza, pia anatajwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.