Pata taarifa kuu
UINGEREZA-USHIRIKIANO

Hatua za kwanza kuelekea kutuliza mvutano kati ya Paris na London

Baada ya mvutano mkali wa siku kumi, Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza amezungumza kwa simu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron Ijumaa Septemba 24.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Juni 18, 2020.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Juni 18, 2020. AFP - HANNAH MCKAY
Matangazo ya kibiashara

Boris Johnson ametaka kumhakikishia mwenzake wa Ufaransa licha ya mvutano uliyosababishwa na mzozo wa nyambizi, kipindi cha mwisho cha mfululizo wa mzozo kati ya London na Paris.

"Ushirikiano wa karibu"

Wakati wa mazungumzo ya simu, kiongozi wa serikali ya Uingereza na rais wa Ufaransa "wamebainisha umuhimu wa uhusiano kati ya Ufaransa na Uingereza na wakakubali kushirikiana kwa karibu kte duniani", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Ikulu ya Elysée  ambayo imesisitiza kuwa mpango huo ulitoka London, imebaini kuwa Boris Johnson ameonyesha "nia yake ya kuanzisha tena ushirikiano kati ya Ufaransa na Uingereza, kulingana na maadili yetu na masilahi yetu ya pamoja (tabia nchi, suala la Indo-Pacific, vita dhidi ya ugaidi)".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.