Pata taarifa kuu
UFARANSA-HAKI

Rais wa zamani wa Ufarans Nicolas Sarkozy kukata rufaa dhidi ya hukumu aliyopewa

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema anatazamia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya mjini Paris baada ya kukutwa na hatia leo Alhamisi Septemba 30.

Kifungo hicho Nicolas Sarkozy atakitumikia nyumbani kwake, kwa kuvishwa bangili ya kielekroniki itakayowawezesha maafisa wa gereza kujua wakati wote mahali alipo.
Kifungo hicho Nicolas Sarkozy atakitumikia nyumbani kwake, kwa kuvishwa bangili ya kielekroniki itakayowawezesha maafisa wa gereza kujua wakati wote mahali alipo. Getty Images - Kiran Ridley
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Paris imemhukumu Nicolas Sarkozy kifungo cha mwaka mmoja jela kwa ufadhili haramu wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2012 kuhusiana na kesi ya Bygmalion.

Hukumu ya rais wa zamani wa Ufaransa itaanza kutekelelezwa mara moja, mahakama imesema. Hukumu za kuanzia miaka miwili hadi mitatu na nusu gerezani, zilitolewa dhidi ya wafungwa wenzake 13.

Nicolas Sarkozy, hakuwepo wakati hukumu hiyo iliyotolewa. Kifungo hicho Nicolas Sarkozy atakitumikia nyumbani kwake, kwa kuvishwa bangili ya kielekroniki itakayowawezesha maafisa wa gereza kujua wakati wote mahali alipo.

Mahakama hiyo imesema wakati wa kampeni ya mwaka 2012, Sarkozy alikiuka ukomo wa viwango vya bajeti inayokubalika kwa shughuli hiyo.

Mahakama ya Paris imesema chama cha Sarkozy cha UMP ambacho kimebadilisha jina na kuitwa Republicans, kilijaribu hila ya kuficha uhalifu huo kwa kuandika stakabadhi za bandia. Katika uchaguzi huo Nicolas Sarkozy alishindwa na mgombea wa chama cha kisoshalisti, Francois Hollande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.